Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:08

Marekani kuendeleza vikwazo dhidi ya Burundi


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Marekani imesema Ijumaa itaendelea kutekeleza vikwazo iliyopitisha Novemba 22, 2015 dhidi ya Burundi kutokana na kuendelea kwa hali ya taharuki, ikiwemo uvunjifu wa amani nchini humo.

Imesema ili kukabiliana na tishio hilo vikwazo hivyo vilivyo kuwa vimewekwa lazima viendelezwe baada ya Novemba 22, 2018.

Hali ya usalama nchini Burundi inaendelea kuwa siyo ya kawaida na ni tishio kwa usalama wa taifa na sera ya nje ya Marekani inayotokana na hali halisi nchini Burundi, imesema taarifa ya White House, yenye amri ya kiutendaji lilosainiwa na Rais Donald Trump.

Agizo la Trump limesema kumekuwepo na uvunjaji wa amani dhidi ya raia, ghasia, uchochezi unaopelekea vurugu, na ukandamizaji mkubwa wa kisiasa, ambao unahatarisha amani, usalama, na utulivu wa Burundi na eneo lote.

Trump ameandika katika amri hiyo ya kiutendaji : “Hivyo, kwa mujibu wa kifungu 202(d) ya Sheria ya Dharura ya Kitaifa (50 U.S.C 1622 (d), mimi naendeleza tamko hilo la dharura la amri ya kiutendaji.”

Wakati wa uongozi wa Rais Obama alisaini amri ya kiutendaji iliyotangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa Burundi na rasilmali zao kufuatia uvunjaji wa amani dhidi ya raia, ghasia, uchochezi uliopelekea vurugu, na ukandamizaji mkubwa wa kisiasa, ambao ulikuwa unahatarisha amani, usalama, na utulivu wa Burundi na eneo lote.

XS
SM
MD
LG