Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:17

Wapiga kura Burundi wapitisha marekebisho ya Katiba


Wananchi wa Burundi wakipiga kura ya maoni kituoni, kitongoji cha Buye, Kaskazini mwa Ngozi, Burundi, Mei 17, 2018.
Wananchi wa Burundi wakipiga kura ya maoni kituoni, kitongoji cha Buye, Kaskazini mwa Ngozi, Burundi, Mei 17, 2018.

Wapiga kura nchini Burundi wameunga mkono mabadiliko ya katiba ambayo huenda yakamruhusu rais kushikilia madaraka hadi mwaka 2034.

Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imesema Jumatatu kuwa asilimia 73 ya wapiga kura wameunga mkono mabadiliko katika kura ya maoni iliyofanyika Alhamisi iliyopita.

Marekebisho hayo yanaongeza muhula wa rais kutoka miaka mitano hadi saba na hivyo mara moja yatamwezesha Rais Nkurunziza kugombea kipindi cha mihula miwili zaidi baada ya awamu yake sasa kumalizika mwaka 2020.

Pia kura hiyo imeidhinisha kuwepo nafasi ya waziri mkuu na itamaliza suala zima la mkataba unaotaka kuwepo serikali ya umoja wa taifa kati ya Wahutu na Watutsi.

Katika tamko lake Jumatatu, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje wa Marekani Heather Nauert amesema kuwa mchakato wa kura ya maoni “ ulikuwa na dosari ya kutokuwepo uwazi, kufungiwa kwa vyombo vya habari, na jaribio la kuwashinikiza wapiga kura.”

Burundi ilizifungia idhaa za kimataifa za VOA na BBC siku kumi zilizopita kurusha matangazo nchini humo.

Nauert amesema pia baadhi ya marekebisho ya katiba “yanakwenda kinyume na makubaliano ya msingi katika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa uliofikiwa nchini Arusha,” ambao ulimaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi.

XS
SM
MD
LG