Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:43

Mamilioni wajitokeza Burundi kupiga kura ya maoni


Wananchi wa Burundi wakiwa wanasubiri kupiga kura Alhamisi, Mei 17, 2018.
Wananchi wa Burundi wakiwa wanasubiri kupiga kura Alhamisi, Mei 17, 2018.

Mamilioni ya wananchi wa Burundi wamepiga kura ya maoni Alhamisi katika mchakato wa kupitisha sheria ya marekebisho ya katiba itakayo mruhusu rais aliyeko madarakani Pierre Nkurunzinza kuendelea kuongoza taifa hilo hadi mwaka 2034.

Vyanzo vya habari nchini Burundi vimesema kuwa watu wengi walionekana kusubiri kwenye mistari mirefu nje ya vituo vya kupiga kura katika mji mkuu wa Bujumbura kwa ajili ya kupiga kura hiyo ya maoni.

Kwa sasa katiba ya Burundi inataka kiongozi kutawala katika nafasi ya urais kwa mihula miwili, miaka mitano kila mmoja. Lakini marekebisho mapya yatatoa nafasi kwa rais kubaki madarakani kwa mihula miwili miaka saba kila mmoja.

Kura ya maoni hiyo inawataka wapiga kura kusema "ndiyo" au "hapana" juu ya mabadiliko ya katiba ambayo yatamwezesha Nkurunziza kugombea tena nafasi ya urais kwa miaka saba kuanzia 2020.

XS
SM
MD
LG