Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:13

Tanzania : Magufuli amfuta uwaziri Januari Makamba


Januari Makamba
Januari Makamba

Rais John Pombe Magufuli amemfuta uwaziri Januari Makamba aliyekuwa Waziri wa Mazingira na Muungano nchini Tanzania na badala yake kumteua George Simbachawene kuchukua nafasi hiyo.

Taarifa ya Ikulu ya Tanzania iliyotolewa Jumapili haijaeleza sababu ya Makamba kutenguliwa uwaziri.

Simbachawene ambaye alijiuzulu katika nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini Septemba 2017, baada ya kutajwa katika kashfa ya kuingia mkitaba mibovu ya madini na kuisababishia hasara Tanzania.

Katika hatua nyengine Rais Magufuli amemteua Hussein Bashe, mbunge wa Nzega Mjini, kuwa Naibu Waziri wa Kilimo.

Kupitia mtandao wa Twitter, Makamba ameandika: "Ni kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo."

XS
SM
MD
LG