Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:08

Azory namba nne kati ya waandishi 10 walioshambuliwa duniani


Azory Gwonda
Azory Gwonda

Mwandishi wa habari wa Tanzania Azory Gwanda ameorodheshwa katika orodha ya waandishi 10 walioshambuliwa duniani.

Orodha iliyochapishwa katika gazeti la Washington Post la Marekani toleo la Julai 1, imemweka Azory Gwanda kama namba nne katika orodha ya waandishi 10 walioshambuliwa, mwandishi wa kwanza akiwa Jamal Khashoggi wa Saudi Arabia aliyeuawa ndani ya ubalozi wa Saudi Arabia nchini Uturuki.

Orodha hiyo imetayarishwa na ushirika wa One Free Press ambao unashirikiana na vyombo kadha likiwemo gazeti la Washington Post la Marekani kushinikiza juhudi za kupata ufumbuzi wa kesi za waandishi hao.

Orodha hiyo yenye waandishi kutoka nchi kadha duniani inajumuisha waandishi wengine wawili wa Afrika, Jones Abiri wa Nigeria ambaye amekamatwa na polisi katika hali ya utatanishi, na mwandishi wa Eritrea Seyoum Tsehaye ambaye yupo gerezani kwa karibu miaka 20 kutokana na kazi za uandishi.

Azory Gwanda mwandishi wa kujitegemea aliyekuwa akiripotia gazet la Mwananchi alitoweka Novemba 21, 2017, maeneo ya Kibiti mkoani Pwani baada ya kuchukuliwa kwenye gari na watu wanaodhaniwa kuwa maafisa wa serikali ya Tanzania. Siku hiyo ilikuwa ni mara ya mwisho Gwanda kuonana na familia yake na rafiki zake kwa mujibu wa utafiti wa kamati inayotetea waandishi wa habar duniani, CPJ.

Waandishi wengine katika orodha ya 10 walioshambuliwa duniani wanatokea nchi za Mexico, Iran, Ukraine, India, Malta na China.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC

XS
SM
MD
LG