Katika mahojiano na shirika la habari la BBC kipindi cha Focus on Africa siku ya Jumatano, Kabudi alisema kuwa Gwanda alitoweka na kufa kwenye eneo Rufiji, mashariki mwa Tanzania.
Aliongeza kuwa tangu kisa hicho kutokea serikali imeweza kudhibiti hali na hasa kwenye eneo la tukio.
Gwanda alitoweka Novemba 21, 2017 baada ya kufuatilia habari kuhusu mauaji ya kutatanisha pamoja na kutoweka kwa watu miongoni mwa jamii yake.
Kwa mujibu wa kamati ya CPJ, hadi sasa serikali haijatoa maelezo kufuatia ahadi yake ya kuchunguza kisa hicho.
Kabudi aliongeza kwamba serikali ya Tanzania haijafurahishwa na kupotea kwa watu pamoja na mauaji ya Rufiji ambayo anasema yametokea kwa maafisa wa polisi pamoja na viongozi wa kisiasa na kwamba wanafanya kila wawezalo kuhakikisha usalama wa raia pamoja na waandishi wa habari.
-Imetayarishwa na Mwandishi wa VOA, Harrison Kamau.