Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:33

Tanzania, China zashindwa kukubaliana juu ya mradi wa bandari ya Bagamoyo


Rais John Pombe Magufuli
Rais John Pombe Magufuli

Mpango wa mradi wa ujenzi wa bandari nchini Tanzania unaoungwa mkono na China utakaogharimu dola za Marekani bilioni 10 umegonga ukuta, wakati pande zote mbili zikihitalafiana juu ya masharti ya uwekezaji huo wa miundombinu, afisa wa ngazi ya juu wa bandari, Tanzania, amesema Jumatano.

Mwaka 2013, Tanzania ilisaini muundo wa mkataba na kampuni ya China Merchant Holdings International, mwendeshaji mkubwa kuliko wote wa bandari ya China, kujenga bandari na zoni maalum ya kibiashara ambayo inalengo la kuibadilisha nchi hiyo ya Afrika Mashariki kuwa ni kituo cha biashara cha kieneo na usafirishaji.

“Masharti waliotupa hayana tija ya kibiashara. Tukasema hapana, tutafute njia ya kufikia makubaliano,” Deusdedit Kakoko, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Tanzania linaloendeshwa na serikali ameiambia Shirika la habari la Uingereza Reuters.

“Hiyo ingekuwa hasara… hawatakiwi kutufanya sisi kama watoto wa shule na kujifanya wao ni waalimu.”

Serikali ya Tanzania imewaandikia rasmi waendeshaji wa bandari ya China juu ya kupinga masharti hayo, Kakoko amesema. “Tunasubiri waanze mazungumzo mapya. Wakati wakiwa tayari, sisi tutaanza mazungumzo.”

Reuters iliwasiliana na makao makuu ya Kampuni ya kimataifa ya Merchant Holdings International, Hong Kong na ofisi ya kampuni hiyo iliyoko Tanzania kupata maoni yao lakini hawakuweza kupata jibu mara moja.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China haikutoa jawabu la papohapo walipotakiwa kutoa maoni yao.

Tangu kuchaguliwa kuwa rais wa Tanzania mwaka 2015, serikali ya Rais John Magufuli imeagiza mazungumzo juu ya miradi yote mikubwa ya wawekezaji wa kigeni yafanyike upya ikiwemo uchimbaji madini, gesi asilia, mawasiliano na miundombinu, ikiwa ni sehemu ya msukumo mpya wa kulinda rasilmali za kitaifa.

Mradi wa bandari ya Bagamoyo ulisainiwa mwaka 2013 na serikali ya awamu ya nne ya Rais Jakaya Kikwete, wakati wa ziara aliyofanya Rais wa China Xi Jinping nchini humo.

Mradi huo pia umefadhiliwa na Mfuko Mkuu wa Akiba wa Serikali ya Oman. Wabunge walitaka maelezo kutoka serikalini wiki iliyopita juu ya sababu za kuchelewa kutekelezwa kwa mradi huo.

Sherehe kubwa za kupokea mradi huo zilifanyika mwisho wa mwaka 2015 lakini ujenzi wa mradi huo bado haujaanza.

Ujenzi wa bandari hiyo Bagamoyo, wenye eneo la kilomita 75 (maili 47) kaskazini mwa Dar es Salaam ungeipa hadhi zaidi bandari ya Tanzania kwa kuipiku bandari ya Kenya iliyoko Mombasa, mlango wa biashara wa Afrika Mashariki, kilomita 300 (maili 180) kaskazini. Bandari ya Bagamoyo itakuwa na eneo la viwanda na reli na barabara zinazounganisha eneo lililokuwa na matumaini ya kuchimba mafuta na kugundua gesi.

Mradi huo unakusudia kupunguza msongamano bandarini katika makao makuu ya kibiashara Dar es Salaam na kubadilisha eneo lililokuwa limetelekezwa kuwa ni kiungo cha biashara na viwanda.

Hata hivyo kuna matatizo ya kiutendaji, na la chini kabisa ni kuwa bandari ya Bagamoyo, kinyume cha ile ya Dar es Salaam, inawezekana ikahitaji zaidi uchimbaji wa kina kikubwa zaidi na zoezi hilo kufanyika mara kwa mara.

XS
SM
MD
LG