Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:09

Viongozi wa EAC wakutana wakati kuna mivutano, vita vya kibiashara, upungufu wa fedha


Viongozi wa Afrika Mashariki
Viongozi wa Afrika Mashariki

Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) walikutana Ijumaa wakati wingu nene la masuala kadhaa ya muda mrefu yaliyo kuwa bado hayajapatiwa ufumbuzi yakiwakabili ikiwemo mivutano ya kibiashara, ushuru na vikwazo ambavyo sio ushuru na changamoto za kukosekana fedha zikiendelea kuikabili jumuiya hiyo.

Hayo yameripotiwa na gazeti la The East African wakiongeza kuwa upande wa Kenya na Tanzania, mazungumzo juu ya mgogoro wa sukari na tumbaku yalikwama baada ya sekretarieti ya EAC kutuhumiwa kushindwa kutatua baadhi ya mambo yaliyokuwa yakisubiri ufumbuzi kwa kipindi cha miezi saba.

Wachambuzi wanaeleza kuwa hivi karibuni Rwanda imekabiliwa na mfukuto wa mvutano wa kidiplomasia baina yake na Burundi na Uganda juu ya kero za masuala ya usalama ya muda mrefu ambayo yanahatari ya kutoweza kudhibitiwa.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania John Magufuli walikuwa wanatarajiwa kuzungumzia mvutano unaoendelea wa biashara kati ya viongozi wa serikali tangu pale walipotoa maagizo kuwa tofauti hizo zitafutiwe ufumbuzi wakati wa mkutano wa marais uliofanyika Kampala mwaka 2018, na hadi sasa juhudi hizo zinasuasua au hazikuzaa matunda kabisa.

Chanzo hicho cha habari kimechambua kuwa hatua ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kumkabidhi uwenyekiti Rais wa Rwanda Paul Kagame kunatarajiwa kupunguza mvutano kati ya nchi hizo mbili,wakati huu ambapo matukio kadhaa yamezidisha hali ya tofauti zao.

Moja ya mambo yanayo zungumziwa ni tukio la kuondolewa nchini Uganda raia wa Rwanda Annie Tabura, Mkurugenzi wa ngazi ya juu wa shirika la simu MTN, kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa la Uganda.

XS
SM
MD
LG