Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:17

Museveni kutafuta hatma ya Mkataba wa EPA Brussels


Yoweri Museveni
Yoweri Museveni

Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA) baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Nchi za Umoja wa Ulaya (EU), bado halijapatiwa ufumbuzi mpaka hivi sasa.

Baada ya Tanzania na Uganda kugoma kusaini mkataba huo wa ushirikiano ambao baadhi ya viongozi wanaufananisha na ukoloni mambo leo, viongozi hao wamekubaliana kutuma ujumbe mjini Brussels, Ubelgiji yaliko makao makuu ya EU ili kujadili kwa kina juu ya EPA na kufikia ufumbuzi.

Mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo ambaye pia ni Rais wa Uganda, Yoweri Museveni atakwenda huko ili kujadili nafasi ya kiuchumi ya EAC na pia kuzungumzia suala la kutoiadhibu Kenya kutokana na nchi wanachama kutosaini mkataba huo.

Akizungumza katika mkutano wa 18 wa wakuu wa nchi za EAC mara baada ya kukabidhiwa kijiti cha kuiongoza jumuiya hiyo na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Rais Museveni alisema, ataongoza ujumbe huo ndani ya mwezi kuanzia jana na kwamba EU haipaswi kuiadhibu Kenya kwa nchi wanachama kutosaini mkataba wa EPA.

“Tutawezaje kujadili na kusaini mkataba hali ya kuwa mwanachama wetu mmoja amewekewa vikwazo na EU ? bado tunahitaji ufafanuzi juu ya mambo kadhaa yaliyomo kwenye mkataba wa EPA,” alisema Museveni.

Museveni ameeleza pia kutofurahishwa na hatua ya Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo Burundi bila kushauriana na viongozi wa jumuiya hiyo. Alisema Burundi ni tatizo la jumuiya hiyo, hivyo wanaweza kulimaza wenyewe.

XS
SM
MD
LG