Wawakilishi wa nchi hizo tatu za Afrika Mashariki (EAC) walipinga juhudi za Jumuiya ya kibiashara ya Marekani juu ya kuwazuia wao kutumia fursa ya kibiashara iliokuwepo kati ya Afrika na Marekani ijulikanayo kama Agoa.
Jumuiya ya biashara ya nguo, inayo julikana kama Smart ilifungua kesi dhidi ya vyombo vya serikali vya biashara nchini Marekani mwezi March vikisisitiza kuwa nchi hizo tatu, pamoja na nchi nyingine mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Kenya, zichukuliwe kuwa hazistahili kupata fursa ya kuuza bidhaa za nguo zisizotozwa ushuru (na usafirishaji wa bidhaa hizo) katika soko la Marekani.
Lawrence Bogard, Mwanasheria anaye wakilisha Smart, ameonya Jumatano wakati wa mahojiano na serikali kuwa makampuni ambayo ni wanachama wa Smart watapata hasara kubwa katika soko la ajira na mapato iwapo upigaji marufuku uingizaji wa nguo za mitumba utatekelezwa kikamilifu na EAC.
Bogard ametaka kwamba Kenya iwekwe katika nchi za EAC ambazo zitapoteza maslahi ya Agoa.
Wakala wa ngazi ya juu wa biashara Marekani alitangaza mwezi uliopita kuwa Kenya haitoingizwa katika nchi ambazo zinauwezekano mkubwa wa kukabiliwa na kufanyiwa tathmini iwapo zinastahili kushiriki kwenye Agoa.
Uamuzi huo uliangalia “hatua zilizochukuliwa na Kenya ikiwemo ile ya kupunguza ushuru, kuanzia Julai 1, 2017 na kuwa tayari kutopiga marufuku uingizaji wa mitumba kupitia hatua za kisera ambazo zinakandamiza biashara zaidi ya inavyotakikana kwa ajili ya kulinda afya ya binadamu.
Lakini mwakilishi wa Smart amependekeza Alhamisi kuwa Kenya ni lazima na yenyewe iwekwe katika thathmini ya fursa ya Agoa mpaka pale maafisa Nairobi watakapotoa ufafanuzi juu ya utayari wa kufuata taratibu za Agoa.
Smart imeweka wazi inataka uthibitisho kuwa ripoti ya Kenya kuweka ushuru wa chini kwa makontena ya mitumba “ hautotekelezwa katika namna ambayo itakinzana na utaratibu wa kuongeza ushuru ulioanzishwa Julai 1 na Kenya,” Bogard amesema.
Kenya itapata hasara zaidi iwapo itazuiliwa fursa ya kusafirisha bidhaa za nguo bila ya ushuru katika programu ya Agoa kuliko nchi yoyote nyingine katika Afrika Mashariki.
Kenya iliuza nguo zenye thamani ya Dola za Marekani milioni 394 katika soko la Marekani mwaka jana, ikilinganisha na jumla ya Dola milioni 43 ya biashara ya Agoa iliofanywa na Rwanda, Tanzania na Uganda.
Ubalozi wa Kenya jijini Washington umesema kuwa ajira 66,000 za Kenya zinatokana na biashara ya kusafirisha nguo kupitia Agoa.