Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 06, 2025 Local time: 16:42

Kumbukumbu ya Hayati Rais Magufuli : Maombi na kuuaga mwili

Hayati Rais John Pombe Magufuli ambaye alifariki Jumatano jioni nchini Tanzania kutokana na maradhi ya moyo, atakumbukwa kwa mengi hasa juhudi alizofanya katika kuleta maendeleo Tanzania katika muda mfupi wa utawala wake.

Mwili wa hayati Magufuli uliifikishwa kanisani na kupelekwa uwanja wa Taifa Jumamosi. Mamia ya wakazi wa Dar es Salaam wamejitokeza sehemu mbalimbali barabarani kutoa heshima zao wakati mwili wa Hayati Magufuli ukipitishwa.

Lakini pia atakumbukwa katika siku hizi za mwisho za maisha yake kwa msimamo mkali kuhusu janga la Covid-19 ambalo limeutikisa ulimwengu kwa kusema Tanzania imefanikiwa kutokomeza virusi vya corona kwa sala na kutumia dawa za miti shamba na hivyo kuwataka wananchi wasiwe na khofu kamwe Covid haitaliyumbisha taifa.




Pandisha zaidi

Makundi

XS
SM
MD
LG