Makamanda wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakitembelea maeneo ambayo yameshambuliwa na waasi wa M23 na kusababisha wakaz kukimbia makazi yao. Wakati huo huo jeshi la DRC limepeleka wanajeshi wake kukabiliana na waasi wa M23. Sehemu ya kwanza ya habari katika picha. Picha zote na Mwandishi wa VOA Austere Malivika.
Jeshi la DRC lapeleka wanajeshi kuzuia mashambulizi ya waasi wa M23 eneo la Karenga
Mkuu wa Jeshi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jenerali Mbangu Masita pamoja na Makamu wake Jenerali Mutu Peke wakisimamia kuwapanga wanajeshi kuzuia waasi wa M23 walioshambulia kijiji cha Karenga, DRC.

1
Mkuu wa Jeshi mashariki mwa DRC Jenerali Mbangu Masita pamoja na makamu wake Jenerali Mutu Peke wakikagua maeneo yaliyoshambuliwa na waasi wa m23. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika

2
Mkuu wa Jeshi mashariki mwa DRC Jenerali Mbangu Masita pamoja na makamu wake Jenerali Mutu Peke wakishauriana. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika

3
Wanajeshi wa DRC wapelekwa katika eneo lililoshambuliwa na waasi wa M23. Picha na mwandishi wa VOA Austere Malivika

4
Wananchi wakilazimika kuhama makazi yao baada ya waasi wa M23 kushambulia vijiji vyao