Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:54

Amnesty International yaitaka Burundi kuwaachia huru waandishi wa habari


Waandishi wa habari na dereva wao ambao wamekamatwa nchini Burundi
Waandishi wa habari na dereva wao ambao wamekamatwa nchini Burundi

Vyombo vya usalama Burundi vimetakiwa mara moja na bila ya masharti kuwaachia huru waandishi wa habari wanne na dereva wao, kwani hawana kosa lolote zaidi ya kuwa walikuwa wanatekeleza majukumu yao.

Kulingana na taarifa iliyotolewa Alhamisi na shirika la haki za bindamu Amnesty International, waandishi hao ni Christine Kamikazi, Agnes Ndirubusa, Terence Mpozenzi na Egide Harerimana ambao wanafanya kazi katika shirika la habari binafsi la Burundi (Iwacu), na dereva wao Adolphe Masabarakiza, walikamatwa Jumanne Octoba 22 wilaya ya kaskazini magharibi ya Musigati, katika jimbo la Bubanza.

Walikuwa wanasafiri kuelekea Bubanza baada ya kupokea taarifa za mapigano yaliotokea kati ya kikundi chenye silaha na majeshi ya jimbo hilo.

Kwa mujibu wa Iwacu, pamoja na waandishi hao na dereva wao kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama juu ya kusudio lao la kusafiri kuelekea eneo hilo, makao makuu ya operesheni ya usalama katika eneo hilo iliamrisha wakamatwe.

Walikuwa wameshikiliwa kuanzia Octoba 24, kwa siku mbili katika kituo cha polisi cha Bubanza.

Walihojiwa na polisi Octoba 23, lakini mpaka sasa hawajafunguliwa mashtaka ya uhalifu wowote.

Kuwakamata waandishi kwa kuwa tu wametekeleza majukumu yao ni jaribio la kukandamiza uhuru wa habari na haki ya uhuru wa kujieleza nchini Burundi.

XS
SM
MD
LG