Kufuatia hatua hiyo hakuna tamko lolote lililotolewa kuhusiana na amri hiyo ya mahakama.
Kulingana na taarifa ya serikali ya Tanzania wanasheria wake tayari wamewasili nchini Afrika Kusini kutafuta ufumbuzi wa suala hilo na kuwa watatoa taarifa kamili mchakato huo utakapomalizika.
Ndege hiyo ilikuwa inatoka Afrika Kusini kwenda jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo Air Tanzania imewaomba radhi wateja wake kupitia mtandao wake wa Twitter kutokana na usubufu walioupata kutokana na kuzuiliwa ndege hiyo na itafanya marekebisho ya safari zake.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.