Serikali pia inakosolewa kwa kitendo cha mtu kubadilishiwa mashtaka na mamlaka za sheria, hali inayotoa wasiwasi mkubwa kwa mustakabali wa haki za binadamu nchini humo.
Aidha tukio la kukamatwa kwa Erick Kabendera, mwandishi wa habari anayeandikia vyombo vya habari ndani na nje ya nchi, katika mazingira ya kutatanisha, na mwenendo wa shauri lake kugubikwa na utata, balozi za Marekani na Uingireza zimeitaka serikali ya Tanzania kutoa hakikisho la kuheshimu haki za kiraia.
Hii inatokana na Tanzania ilivyotambua kuwa haki za kiraia ni za msingi, pamoja na kuridhia mikataba mbalimbali ya haki za kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, likiwemo azimio la kimataifa la haki za Rai na Kisiasa.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.