Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:14

Tanzania : Hatimaye polisi wathibitisha kumkamata Erick Kabendera


Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Ki-moon akizungumza na mwandishi wa habari Erick Kabendera Octoba 2008.
Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Ki-moon akizungumza na mwandishi wa habari Erick Kabendera Octoba 2008.

Hatimaye mwandishi anayeandikia magazeti ya ndani na nje nchini Tanzania Erick Kabendera imethibitishwa kuwa anashikiliwa na polisi.

Mtandao wa Millardayo.com Jumatatu umekariri jeshi la polisi likisema kuwa mwandishi huyo anashikiliwa na jeshi hilo na watatoa taarifa zake kamili Jumanne.

Siku ya Jumatatu jioni ripoti ya gazeti la Mwananchi linalochapishwa nchini zilieleza kuwa watu hao ambao walishuhudiwa na majirani walimteka nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni.

Awali Jeshi la polisi lilikanusha kuwa na taarifa za kukamatwa kwa Kabendera wakisema hawana taarifa ya tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Dar es Salaam nchini Tanzania, Mussa Taibu pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa waliliambia gazeti la Mwananchi watafuatilia kadhia hiyo.

Mmoja wa wana ndugu ambaye ameomba jina lake lisitajwe amesema, “Kabendera amechukuliwa na watu sita ambao walifika nyumbani kwake na kuingia kwa nguvu wakiwa na gari aina ya Toyota Alphard.”

“Watu hao walijitambulisha lakini hawakutoa vitambulisho vyao na kuingia kwa mabavu ndani ya nyumba na wala hawakuficha nyuso zao na walisema wanamchukua (Kabendera) wanampeleka Polisi Oysterbay. Kabla ya kuondoka, walichukua simu ya Kabendera na ya mke wake,” amesema Loy Kabendera ambaye ni mke wa Erick.

XS
SM
MD
LG