Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:30

Mwandishi wa habari atekwa Tanzania


Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Ki-moon akizungumza na mwandishi wa habari Erick Kabendera Octoba 2008.
Katibu Mkuu mstaafu wa Umoja wa Mataifa Ki-moon akizungumza na mwandishi wa habari Erick Kabendera Octoba 2008.

Mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera aliyeripotiwa kuchukuliwa kwa nguvu na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi.

Kulingana na ripoti ya gazeti la Mwananchi linalochapishwa nchini watu hao ambao walishuhudiwa na majirani walimteka nyumbani kwake nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam eneo la Mbweni.

Kabendera ambaye anaandikia magazeti ya ndani na nje ya Tanzania, inaelezwa ametekwa Jumatatu jioni.

Mmoja wa wana ndugu ambaye ameomba jina lake lisitajwe amesema, “Kabendera amechukuliwa na watu sita ambao walifika nyumbani kwake na kuingia kwa nguvu wakiwa na gari aina ya Toyota Alphard.”

“Watu hao walijitambulisha lakini hawakutoa vitambulisho vyao na kuingia kwa mabavu ndani ya nyumba na wala hawakuficha nyuso zao na walisema wanamchukua (Kabendera) wanampeleka Polisi Oysterbay. Kabla ya kuondoka, walichukua simu ya Kabendera na ya mke wake,” amesema Loy Kabendera ambaye ni mke wa Erick.

Loy anasema walimchukua Erick kwa nguvu hali iliyowafanya baadhi ya majirani kufika kushuhudia tukio hilo na wale waliodiriki kupiga picha walinyang’anywa simu zao na askari hao.

Gazeti la Mwananchi limewatafuta Kamanda wa Polisi Kinondoni, Dar es Salaam nchini Tanzania, Mussa Taibu pamoja na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kuhusu taarifa za Kabendera na kwa pamoja wamesema hawana taarifa ya tukio hilo huku wakiahidi kufuatilia.

XS
SM
MD
LG