Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 07:51

Tazama baadhi ya wajumbe muhimu wa baraza la mawaziri la Donald Trump

Wakati utawala wa rais mteule Trump unajumuisha maelfu ya wateuliwa, watu aliowapendekezwa kuunda baraza la mawaziri ni muhimu zaidi.

Baraza hilo la Mawaziri kwa kawaida hujumuisha makamu wa rais na viongozi wa wizara 15 za utendaji, kama vile wizara za Mambo ya Nje na Hazina.

Pia linajumuisha takriban maafisa 10 watakaohudumu katika nafasi za ngazi ya baraza la mawaziri kama vile mwakilishi wa biashara wa Marekani, mkurugenzi wa upelelezi wa taifa na mkuu wa wafanyakazi wa White House.

Isipokuwa makamu wa rais na mkuu wafanyakazi, nafasi nyingine zote zinahitaji uthibitisho wa Seneti.


Makundi

XS
SM
MD
LG