Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 16:07

Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara


Ghana yakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:32 0:00

Ghana inakabiliwa na wimbi la taarifa potofu zenye madhara. Baadhi ya waandishi wa habari wana matumaini ya kukabiliana na hali hiyo kwa kutoa ripoti sahihi.⁣

Mradi wa Media Foundation for West Africa⁣

Kwaku Asante anaongoza timu ya waandishi wa habari wa kuhakiki ukweli, Fact-Check Ghana, mradi wa Media Foundation for West Africa, wenye makao yake katika mji mkuu, Accra.⁣

Timu hiyo ina kazi ngumu ya kupambana na habari potofu na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kawaida.⁣

Asante anasema yeye na wanahabari wenzake wana kazi kubwa ya kufanya kuhusu changamoto hiyo.⁣

Kiongozi wa Timu ya Fact Check⁣

Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact Check Ghana anasema:⁣

“Kuna taarifa nyingi potofu huko nje. Ukiamka asubuhi unakuta kuna mambo mengi yanayoulizwa. Je, unaweza kuliangalia hili kwa ajili yetu? Je, hizi ni taarifa sahihi? Je, hii ni kweli? Kuna yeyote wa kutusaidia? Kisha tunafika na kusema, “ndiyo, tumeichunguza. Huu ndio ukweli. Hii si sahihi, na hii ni taarifa sahihi.”⁣

Kuhakiki ukweli, ni kazi ambayo Asante anaipenda, kwa miaka mitano iliyopita, alifanya kazi kuwajuza raia wa Ghana na taarifa sahihi.⁣

Kwaku Asante, kiongozi wa timu ya Fact-Check Ghana asema: “Inanipa furaha kubwa kujua kwamba unafanya kitu ambacho kinaleta matokeo mazuri na ushawishi wa moja kwa moja kwa watu, kwa sababu habari za uongo zinaweza kuwa na athari mbaya sana, tizama kipindi cha Covid 19 ambapo kulikuwa na mtiririko wa habari za uongo.”⁣

Ripoti ya Isaac Kaledzi, VOA, Accra, Ghana.⁣

Forum

Makundi

XS
SM
MD
LG