Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 27, 2025 Local time: 20:08

Habari Potofu: MISA inawasaidia waandishi Malawi kujenga uaminifu


Habari Potofu: MISA inawasaidia waandishi Malawi kujenga uaminifu
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:25 0:00

Nchini Malawi ambako kuthibitisha habari sahihi kumejaa changamoto, Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika MISA inafanya kazi ili kuboresha usahihi wa kuripoti na kuwasaidia waandishi wa habari kujenga uaminifu.

Gazeti la The Nation

Suzgo Chitete ni mwandishi wa habari za uchunguzi na naibu mhariri mkuu wa gazeti la kila siku la Malawi, The Nation, huko Lilongwe. Kila asubuhi anafika kazini akiwa na imani kwamba uandishi wa habari ni wito wa kutoa taarifa za ukweli kwa wasomaji.

Chitete na waandishi wengine kadhaa wa habari nchini Malawi walihudhuria mfululizo wa mafunzo yanayoangazia ukweli ambayo yanawapa waandishi wa habari ujuzi wa kugundua habari potofu na habari zisizo za kweli.

Suzgo Chitete, Mwandishi wa gazeti la The Nation anaeleza: "Mafunzo haya yameleta mwamko na kutukumbusha kwamba kila tunapoandaa habari, au kila wakati tunapofanya mahojiano na mtu, lazima tuwe makini na taarifa za uongo, ili wasikilizaji wapatiwe taarifa za kuaminika."

Taasisi ya Vyombo vya Habari MISA

MISA Malawi, bodi ya ndani katika Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika, inaendesha programu hizi kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya kimataifa. Mpango wake unaowapatia waandishi wa habari ujuzi wa kuhakiki habari za kweli, unaungwa mkono na Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo ya Habari cha Deutsche Welle. Mwenyekiti wa MISA nchini Malawi, Golden Matonga anaelezea.

Golden Matonga, Mwenyekiti wa MISA Malawi: "Tuna DW Akademie ya Ujerumani ambayo imekuwa ikisaidia kazi zetu za msingi katika MISA Malawi kwa misingi ya kujenga uwezo wa miradi kwa waandishi wa habari wa Malawi. Tunashirikiana na UNESCO kuangalia kusaidia ripoti za uchaguzi kwa ujumla ambapo pia imewezesha kufikia maeneo ya kuangalia ukweli kuhusu taarifa."

Matonga anasema mradi wa Elimu ya Uandishi wa Habari wa MISA Malawi unatoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa Malawi ili kuzuia kuenea kwa taarifa potofu na za uongo ambazo ni muhimu hasa wakati nchi inapojiandaa kwa uchaguzi mkuu 2025.

Golden Matonga, Mwenyekiti wa MISA Malawi anasema: Hivi karibuni tulishuhudia kifo kibaya cha makamu wa rais na kuna habari nyingi za uongo ambazo zilisambaa kuhusu kile kilichotokea katika ndege iliyoanguka. Matukio haya yanatukumbusha jinsi habari za uongo zinavyoweza kuwa hatari. Tunaelekea kwenye uchaguzi. Hapo awali tulikuwa na uchaguzi wa wabunge 2019 na uchaguzi wa rais 2020. Kisha tukaanza kuona tena mwenendo wa habari za uongo zinazoathiri nafasi ya kisiasa.

Ukweli wa Wanasiasa

Maeneo ya kuzingatia ni pamoja na kuangalia ukweli wa wanasiasa, na madai yanayohusiana na uchaguzi, na kuthibitisha maudhui ya vyombo vya habari kama vile picha na video kwa kutumia zana kama vile Google Image Search.

Kituo cha Radio Islam

Mtangazaji wa Redio, Shakira Juma anasema anaziangalia taarifa zinazotumwa kwenye mitandao ya kijamii kwa mashaka.

Shakira Juma, Mtangazaji wa Radio Islam: "Ninachagua kuhusu habari ambazo ninaziamini , au la, kwa sababu ya habari za uongo katika mitandao ya kijamii, machapisho bandia ambayo yanatokea siku hizi. Hivyo ndivyo hali ilivyo. Siwezi kuamini chochote."

Wasemavyo Wakufunzi

Wakufunzi wanasema habari za uongo zimekithiri nchini Malawi kwa kiasi kikubwa kutokana na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao wanakimbilia kuwatapeli waandishi wa habari kwa kuchapisha habari ambazo hazijathibitishwa, za udanganyifu, au hata kuvumbuliwa. Chisomo Kachapila anatoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu namna ya kuangalia taarifa za ukweli nchini Malawi.

Chisomo Kachapila, Mkufunzi wa Ukaguzi kujua Habari za Ukweli:"Kwa sababu pia wakati mwingine kama vyombo vya habari, tumeangukia katika mtego huu, ambapo taarifa tunazosema ni za wale ambao wako katika uongozi. Hatuzungumzii taarifa zinazowahusu watu. Kwa hivyo hivi sasa watu, watazamaji wamekuwa waandishi wa taarifa zao wenyewe. Kwa hivyo, shida iliyopo ni kwamba hawana ufahamu kuhusu vyombo vya habari. Tumeona picha walizopiga, picha za kutisha walizochapisha. Hawajui madhara yaliyopo katika maadili."

Kachapila anasema kuwa kudukua habari za uongo imekuwa changamoto kwa sababu kuna taarifa chache sana kuhusu habari za ndani katika nchi za Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Chisomo Kachapila, Mkufunzi wa Ukaguzi unaoangazia Habari za ukweli anasema: "Kwa hivyo, kwa mfano, ukipiga picha ambayo ilichukuliwa katika ulimwengu wa Magharibi, utagundua kwamba ukienda na kuiangalia ili upate uthibitisho, ni rahisi kufanya hivyo. Tunahitaji taarifa zaidi zinazotuhusu sisi kutoka Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara, kutoka Kusini mwa Afrika, kwenye mtandao, ili kurahisisha kazi hii. Vinginevyo, sio rahisi kufanya uchunguzi kujua ukweli wa taarifa katika muktadha wetu kama ilivyo katika ulimwengu wa Magharibi."

Chitete anasema mafunzo hayo yamemsaidia kukua kitaaluma na sasa anatumia ujuzi huo kuwasaidia waandishi wengine wa habari katika kuangalia ukweli wa taarifa kabla ya kuzitoa.

Wasemavyo Waandishi wa Habari

Suzgo Chitete, Mwandishi wa Habari gazeti la the Nation anasema:

Kwa sababu nimekuwa makini kila wakati ninapoandaa taarifa, kila wakati ninaposikiliza kauli fulani, hasa kauli za kisiasa, lazima nichunguze ukweli. Lazima nithibitishe mara mbili ili kuwa na uhakika. Kukosekana kwa mafunzo kama hayo, unafahamu kwamba wakati mwingine unatumia fursa inapokuja.

Hata hivyo Chitete anasema baadhi ya mashirika na idara za serikali bado zinasita kutoa taarifa zinazohitajika kuthibitisha habari hizo, na hatua hii ya kuzuia taarifa inatatiza juhudi zao za uandishi.

Suzgo Chitete, Mwandishi wa Habari gazeti la The Nation anaeleza:Kwa mfano, nina masuala na Wizara ya Mambo ya Nje, kwa sababu nilitaka habari kuhusu sifa kwa wanadiplomasia wote walioteuliwa tangu 2020. Suala ni kuona kama kweli wale walioteuliwa wana hadhi ya kutosha kuitumikia Malawi. Serikali imekuwa ikisema. Tunaajiri watu sahihi. Lakini tuna wasiwasi wakati mwingine kwamba hao sio watu sahihi, lakini kisiasa hawa ni watu sahihi.

Tume ya Haki za Binadamu

Katika uamuzi wake, Tume ya Haki za Binadamu ya Malawi, iliyopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa sheria ya upatikanaji wa habari, iliikosoa Wizara ya Mambo ya Nje kwa kukataa kutoa taarifa za umma zilizoombwa na Chitete.

MISA na UNDP

Matonga anasema mbali na mafunzo hayo, MISA Malawi na UNDP pia wanaufanyia kazi mradi mpya ambao utasaidia kuhamasisha taarifa za kuaminika za habari wakati wa uchaguzi mkuu 2025.

Golden Matonga, Mwenyekiti wa MISA Malawi anaeleza: "MISA, kwa upande wetu, tutazindua mradi kamili wa kuangalia taarifa zilizo za kweli kwa msaada kutoka UNDP. Mradi unaitwa “I verify” ambapo tutaweza kuuliza umma kwa ujumla kuripoti kwenye tovuti, kesi za taarifa potofu na zisizo sahihi, na tutakuwa na timu ya wataalam ambao watakwenda na kuondoa taarifa hizo bandia na kushirikisha taarifa sahihi."

Matonga anaamini juhudi hizi zitawapa waandishi wa habari ujuzi na vifaa vinavyoweza kupatikana kwa urahisi ili kuangalia taarifa za ukweli katika uandikaji wa ripoti zao na kuwawezesha wananchi kufahamu wenyewe, ni Habari zipi zenye uhakika na za kuaminika.

Imetayarishwa na Mwandishi Lameck Masina kutoka Lilongwe, Malawi.

Forum

Makundi

XS
SM
MD
LG