Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 21:39

Olimpiki ya aina yake yaanza kwa sherehe za ufunguzi bila ya watu kukaribiana

Baada ya kuchelewa kwa mwaka moja kutokana na janga la Corona, Michezo ya Olimpiki ya Tokyo imeanza rasmi Ijumaa kwa tafrija ya ufunguzi ambayo ilikuwa ndogo lakini imesheherekewa.

Michezo hiyo inafanyika huku viti vya washangiliaji vikiwa vitupu katika Uwanja wa Olimpiki wa Tokyo, ambapo kuna watu muhimu 900 na maafisa wengine wakihudhuria kwa sababu za tahadhari ya maambukizi ya COVID-19

Ufunguzi wa sherehe hizo, ulioitwa "Tumeunganishwa na Hisia," inaweza kuwa moja ya vitu vya kawaida vinavyofanya michezo hii kuwa siyo ya kawaida kabisa kufanyika katika mpangilio huu.


Pandisha zaidi

Makundi

XS
SM
MD
LG