Akiongea katika mkutano wa Geneva, Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, amesema idadi hiyo inaweza kuwa ya juu zaidi kama upimaji ungekuwa wa kutosheleza barani Afrika.
“Wiki iliyopita kumekuwa na ongezeko la asilimia 51 katika taarifa za idadi ya maambukizi zilizo ripotiwa katika bara langu, Afrika, na asilimia 60 ya ongezeko la vifo. Kutokana na changamoto za hivi sasa za kupata vifaa vya kupima COVID-19, inawezekana kuwa idadi halisi iko juu kuliko kile
Hadi kufikia siku ya Ijumaa, takwimu rasmi zinaonyesha, Algeria, ambayo inavifo zaidi ya 360 hadi sasa, ni nchi ya Kiafrika iliyokuwa na idadi ya juu zaidi ya vifo. Misri ni ya pili ikiwa na zaidi ya vifo 200. Morocco imeripoti vifo 135 na Afrika Kusini 50.
Nchi za Kiafrika zimethibitisha kuwa na jumla ya maambukizi 19,334 tangu mlipuko wa virusi hivyo kutokea China mwisho wa mwezi Disemba 2019.
Japokuwa hadi sasa Afrika imekuwa na maambukizi machache ukilinganisha na maeneo mengine ya dunia, maafisa wa afya wanahofia kuwa hali hiyo inaweza kugeuka na kuwa mbaya zaidi.