Idadi ya wahanga wa shambulizi la Somalia yafikia 33

Your browser doesn’t support HTML5

Somalia : Shambulizi la Hoteli ya Medina

Watu 33 wakiwemo wageni wameuawa katika shambulizi la bomu la kujitoa muhanga katika hoteli ya maarufu ya Medina mjini Kismayo, Somalia.

Wanamgambo wa al-Shabaab wanadai kuhusika na shambulizi hilo.

Vyanzo rasmi vya habari vimesema afisa wa ngazi ya juu kimkoa amesema Jumamosi mshambuliaji wa kujitoa muhanga aliigonga gari iliyokuwa na milipuko katika hoteli ya Medina Ijumaa.

Ameeleza kuwa watu kadhaa wenye silaha nzito walilazimisha kuingia ndani ya hoteli hiyo huku wakirusha risasi.

Hoteli hiyo ilikuwa imezingirwa kwa takriban masaa 12 na mapigano kati ya majeshi ya nchi hiyo na washambuliaji hao yalimalizika alfajiri ya Jumamosi.

Taarifa kutoka kwa rais wa jimbo Ahmed Mohamed zinasema kuwa Wakenya watatu, Watanzania watatu, Wamarekani wawili, Muingereza mmoja na raia mmoja wa Canada ni kati ya watu 26 waliouwawa.

Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa Kuna pia raia wawili wa China waliokuwa wamejeruhiwa.

Naye afisa wa usalama wa jimbo hilo Mohamed Abdiweli amesema majeshi ya usalama yamefanikiwa kuudhibiti mji huo na gaidi wa mwisho alipigwa risasi na kufariki.