Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:18

Wanajeshi 8, al-Shabaab 14 wauawa Somalia


Silaha zinazotumiwa na wapiganaji wa al-Shabaab
Silaha zinazotumiwa na wapiganaji wa al-Shabaab

Mapigano kati ya majeshi ya mkoa ya Somali na wapiganaji wa al-Shabaab Jumamosi yameuwa watu sio chini ya 22, walioshuhudia tukio hilo na maafisa wa nchi hiyo wamesema.

Mapigano hayo yaliyotokea Kusini Magharibi ya Somalia yalianza baada ya wapiganaji wa al-Shabaab wenye silaha nzito walivyokuwa wakijaribu kuteka kituo cha jeshi katika mkoa wa Bay.

Afisa wa serikali ya Somalia ameiambia VOA kuwa wanajeshi hao walikuwa katika mapambano makali kwa zaidi ya masaa sita wakiwakabili wapiganaji wa al-Shabaab waliokuwa wameshambulia kambi ya jeshi kutoka pande nne.

“Walitushambulia kutoka maeneo manne ili waweze kuteka kambi mnamo majira ya saa moja asubuhi saa za hapa Somalia, baada ya masaa matano ya mapambano tuliweza kuwazuia na kulazimisha kukimbia,” amesema Kanali Osman Nurow.

Nurow amesema majeshi ya serikali yaliyotumwa kutoka mji wa karibu wa Baidoa ili kusaidia kituo hicho waliingia katika mapambano hayo mara moja, na kuweza kuwauwa wapiganaji wasiopungua 14.

Rais wa mkoa aliyechaguliwa Abdiaziz Hassan Mohamed, pia anajulikana kama Lafta Gareen, amesema majeshi ya mkoa huo yalipoteza wanajeshi nane katika mapambano hayo.

XS
SM
MD
LG