Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:09

Walio jeruhiwa katika shambulizi la Somalia wafikia 54


wanajeshi wa kulinda amani ya Umoja wa Afrika (AMISOM) kutoka Burundi wakifanya doria Mogadishu
wanajeshi wa kulinda amani ya Umoja wa Afrika (AMISOM) kutoka Burundi wakifanya doria Mogadishu

Maafisa nchini Somalia wanasema idadi ya waliojeruhiwa imeongezeka kufikia 54, na idadi ya waliokufa hadi sasa 30.

Mukhtar Dhaga-cadde, mkurugenzi wa mawasiliano ya umma wa mkoa wa Benadir amethibitisha idadi hiyo.

Mlipuko wa Jumamosi ulilenga kituo cha ukaguzi wa usalama karibu na kituo cha kitaifa cha Sanaa karibu na makazi ya rais. Mlipuko wa pili ulitokea katika eneo la karibu.Kikundi cha Al-Shabab kimedai kuhusika na mashambulizi hayo.

Polisi siku ya Jumamosi wameeleza kuwa watu saba waliuwawa baada ya milipuko hiyo miwili mjini Mogadishu, ambayo kundi la wanajihadi wa Al-Shabaab walidai kuhisika na shambulizi hilo.

Amesema idadi ya vifo imeongezeka baada ya baadhi ya wale waliojeruhiwa kufa wakiwa hospitali.

Pande zote raia na vikosi vya usalama ni kati ya wale walioathirika na shambuliz hilo, maafisa wamesema.

Kituo cha Televisheni cha Somalia kinacho endesha shughuli zake Uingereza kimesema kuwa watatu kati ya wafanyakazi wake ni miongoni wa waliouwawa, wakimtaja mmoja wao Awil Dahir kuwa aliokuwa na uraia pacha wa Somalia na Uingereza.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amelaani “mashambulizi yasiyo kuwa na ushujaa”.

“Tutaendelea kuwashinda magaidi ili tuweze kuongoza wananchi wa Somalia kwenda kwenye utulivu na mafanikio,” amesema katika tamko lake.

Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khaire aliwatembelea wale wote waliojeruhiwa.

XS
SM
MD
LG