Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:47

Utafiti unaonesha vifo vinayo tokana na ugaidi vyapungua


Ripoti ya hali ya ugaidi duniani, 2018
Ripoti ya hali ya ugaidi duniani, 2018

Vifo vilivyo sababishwa na ugaidi vimepungua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita duniani, tafiti mpya iliyohusisha nchi zote duniani imegundua.

Tafiti ya sita ya kila mwaka juu ya hali ya ugaidi duniani, iliochapishwa na Taasisi yenye kuangalia hali ya uchumi na amani yenye ofisi zake Sydney (IEP), imesema vifo vinavyotokana na ugaidi vimepunguwa duniani kwa asilimia 27 mwaka 2017, ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo idadi ya vifo hivyo kupungua.

Hata hivyo, ugaidi umebaki kuwa ni tishio kubwa kwa usalama wa dunia, ripoti hiyo imeeleza.

Ripoti hiyo inaonyesha kuwa mashambulizi ya kigaidi mengi yanaziathiri nchi ambazo zinavurugu nyingi za kisiasa.

Nchi kumi ambazo zimeathiriwa zaidi na ugaidi ni Afghanistan, Iraq, Nigeria, Somalia, Syria, Pakistan, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na India.

“Migogoro na ugaidi wa kitaifa ni njia kuu za kusababisha ugaidi,” ameandika Steve Killelea, mwenyekiti mtendaji wa IEP.

Maeneo yaliyo hatarishi katika ugaidi “yote yalihusika kwa angalau mgogoro mmoja wenye uvunjifu wa amani, na nane yaliingia katika vita kubwa na kusababisha vifo sio chini ya 1,000. Hizi nchi 10 zilichangia asilimia 84 ya vifo vilivyotokana na ugaidi mwaka 2017,” repoti hiyo imeeleza.

XS
SM
MD
LG