Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:06

Marekani yatafakari kufunga vituo vya kupambana na ugaidi Afrika


Picha za wanajeshi kikosi maalum cha jeshi la Marekani kutoka kushoto Sergent Jeremiah Johnson, Sgt. Bryan Black, Sgt. Dustin Wright na Sgt. La David Johnson. Wanajeshi hawa waliuwawa Niger, Afrika Magharibi, Octoba 4, 2017.
Picha za wanajeshi kikosi maalum cha jeshi la Marekani kutoka kushoto Sergent Jeremiah Johnson, Sgt. Bryan Black, Sgt. Dustin Wright na Sgt. La David Johnson. Wanajeshi hawa waliuwawa Niger, Afrika Magharibi, Octoba 4, 2017.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) inatafakari kuwaondosha takriban makomando wa Marekani wote kutoka Niger na kufunga vituo vya kupambana na ugaidi katika bara la Afrika, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari.

Maafisa wa Pentagon wameliambia gazeti la The New York Times kuwa vituo vya kijeshi vya Marekani huko Cameroon, Kenya, Libya na Tunisia pia vitafungwa iwapo Waziri wa Ulinzi Jim Mattis atapitisha mpango huo, lakini Marekani itaendelea kuwa na uwepo wa kikosi kikubwa cha jeshi lake Nigeria na Somalia.

Kwa mujibu wa The Times, hatua hiyo ni sehemu ya kubadilika kwa mkakati wa Marekani kutoka kupambana na vikundi vya waasi na kuangalia uwezekano wa kuangaza mapigano makubwa.

Jambo hilo limeibuka baada ya shambulizi dhidi ya wanajeshi wa Marekani huko Niger mwaka 2017 ambalo liliwauwa wanajeshi wa Marekani wanne, ambapo Pentagon ilikiri kuwa kulikuwa na udhaifu upande wao.

Magazeti yanaripoti mamia ya wanajeshi wa Marekani barani Afrika watapangiwa kazi upya chini ya mpango huu.

Hata hivyo Jenerali Thomas Waldhauser, mkuu wa kikosi cha maalum cha Marekani Afrika, African Command, siku za nyuma aliliambia The Times kwamba Marekani “haitajiondoa” na haitatelekeza jukumu lake la kuwafundisha wanajeshi wa nchi hizo jinsi ya kupambana na ugaidi.

Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Ulinzi wanapinga mpango huo wa kufunga vituo vya kijeshi Afrika, wakisema inaweza kupunguza ushawishi wa Marekani na Afrika wakati ambao China na Russia inaangaza kuimarisha ushawishi huo.

Lakini afisa moja ameiambia The Times kuwa nchi za Kiafrika tayari zimejenga uwezo wake mkubwa wa kijeshi wa kupambana na ugaidi na wengi wao hawahitaji uwepo wa kudumu wa Marekani.

XS
SM
MD
LG