Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 09:59

Marekani yaadhimisha mashambulizi ya 9/11


Maadhimisho ya mashambulizi ya kigaidi mjini New York, yaliyofanyika Sept. 11, 2018.
Maadhimisho ya mashambulizi ya kigaidi mjini New York, yaliyofanyika Sept. 11, 2018.

Wamarekani Jumanne waliadhimisha miaka 17 tangu mashambulizi ya kigaidi ya tarehe 11 mwezi Septemba mwaka wa 2001 yaliyosababisha vifo vya takiban watu 3,000 na wengine kujeruhiwa katika majimbo ya New York, Virginia na Pennsylvania.

Rais Donald Trumpo alihudhuria moja ya hafla za maadhimisho hayo kwenye kumbukumbu iliyojengwa mjini Shanksville, Pennsylvania, karibu na eneo ambapo ndege ya abiria ya United Airlane, nambari 93, ilianguka, baada ya abiria wapatao 40 na wafanyakazi wa ndege kuchukua udhibiti wakekutoka kwa watekaji waliokuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al-Qaeda.

Trump alisema ndege hiyo ilianguka dakika ishirini tu kutoka mji mkuu Washington DC, na kwamba kama si ujasiri wa abiria hao, Mrekani ingeshuhudia janga kubwa hata Zaidi kama chombo hicho kingefika mjini Washington.

Maadhimisho mengine kama hayo yalifanyika kwenye makao makuu ya kijeshi, ya Pentagon, jimbo la Virginia na mjini New York, ambako watu wengi Zaidi walikufa baada ya majengo mawili makubwa kushambuliwa na watekaji waliokuwa wanaendesha au walioamrisha marubani wa ndege za abiria kushambulia majengo hayo

Mashambulizi hayo yalitekelezwa na wanaume 19 waliokuwa na ushirika na al-Qaida, ambayo yalibadilisha kabisa mtazamo wa Marekani kuhusu usalama na kuipelekea kutangaza vita dhidi ya ugaidi na kuishambulia Afghanistan.

XS
SM
MD
LG