Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 05:03

Somalia imetumbukia katika matatizo mapya ya kisiasa


Rais wa Somalia, Mohammed Abdullahi "Farmajo"
Rais wa Somalia, Mohammed Abdullahi "Farmajo"

Ni baada ya kuibuka hoja ya kumshtaki kumuondoa madarakani Rais Mohammed Abdullahi kwa shutuma za matumizi mabaya ya ofisi kupita kikwazo kimoja muhimu

Somalia imetumbukia katika matatizo mapya ya kisiasa Jumatatu baada ya kuibuka hoja ya kumshtaki kumuondoa madarakani Rais Mohammed Abdullahi kwa shutuma za matumizi mabaya ya ofisi kupita kikwazo kimoja muhimu.

Spika wa bunge la Somalia, Mohammed Mursal Jumapili jioni alikubali hoja iliyotiwa saini na wabunge 92 kati ya 275. kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa AFP waraka huo unamshutumu rais ambaye maarufu kwa jina la “Farmajo” kukiuka katiba kwa kujihusisha na waraka wa siri wa maelewano na mataifa ya kigeni.

Hoja hiyo inafafanua juu ya udhibiti wa bandari za Somalia na kuungana na nchi za Ethiopia na Eritrea. Hoja hiyo iliwasilishwa mwezi mmoja baada ya Farmajo kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed na Rais wa Eritrea Isaias Afwerki kwa mazungumzo juu ya kuimaisha uhusiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo ambayo yalikuwa hasimu. Hoja hiyo itafanikiwa kama wale waliowasilishwa watapata uungaji mkono wa theluthi mbili kati ya wabunge 275 wa bunge la Somalia.

XS
SM
MD
LG