Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 04:46

Waziri wa zamani, raia 4 wauawa katika mlipuko wa bomu Somalia


Gari lililolipuka katika mji mkuu wa Mogadishu, Somalia, Mei 22, 2019.
Gari lililolipuka katika mji mkuu wa Mogadishu, Somalia, Mei 22, 2019.

Polisi nchini Somalia wamesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Hussein Elabe Fahiye ni kati ya watu wasiopungua watano waliouawa wakati bomu lilipo lipuka karibu na ikulu ya rais katika mji mkuu, Mogadishu, Jumatano.

Watu wasiopungua 13 walijeruhiwa pia katika mlipuko huo.

Wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab wamedai kuhusika na mlipuko huo, wakisema kuwa walikuwa wamekusudia kuwaua wanajeshi, wabunge na maafisa wengine wa serikali.

Al-Shabab mara nyingi wamekuwa wakilipua mabomu katika mji huo mkuu karibu na eneo la ikulu ya rais na katika mahoteli ambayo aghlabu wanafikia maafisa wa serikali na wageni.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.
.

XS
SM
MD
LG