Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:43

Magaidi wauwa 28 Somalia


Mwili wa mtu aliyekuwa hajatambuliw katika eneo la mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia, Novemba 9, 2018.
Mwili wa mtu aliyekuwa hajatambuliw katika eneo la mlipuko wa bomu Mogadishu, Somalia, Novemba 9, 2018.

Walipuaji wa kujitoa mhanga wameuwa watu 28 wakiwemo wapiganaji 6, katika mashambulizi matatu ya mabomu ya kutegwa kwenye magari, mjini Mogadishu, Somalia.

Kundi la wapiganaji la Al-shabaab lenye mafungamano na kundi la kigaidi la Al-Qaeda, limedai kuhusika na mashambilizi matatu karibu na hoteli ya Sahafi, iliyo karibu na makao makuu ya ujasusi CID.

Maafisa wa polisi wanasema kwamba walinzi wa hoteli ya Sahafi, waliwafyatulia risasi wahanga baada ya mlipuko na kuuawa wapiganaji wanne waliojaribu kuingia hotelini.

Dakika 20 baadaye, mlipuko wa tatu ukatokea karibu na hoteli hiyo kutokana na bomu lililokuwa limetegwa gwenye gari la miguu mitatu maarufu kama Tuk tuk.

Mumiliki wa hoteli ya Shafi, alichukua usimamizi wa hoteli baada ya babake kuuawa katika shambulizi la wapiganaji mwaka 2015, naye ameuawa katika mashambulizi hayo ya leo ijumaa.

XS
SM
MD
LG