Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 16:21

Bomu lawauwa maafisa usalama 8 Kenya


Kikundi cha kigaidi cha al Shabaab, Somalia
Kikundi cha kigaidi cha al Shabaab, Somalia

Maafisa usalama wasiopungua wanane Jumapili waliuwawa baada ya gari walilokuwa wakisafiria kukanyaga bomu katika eneo la Bojigaras, Kaunti ya Wajir.

Kwa mujibu wa gazeti la the Standard Digital wahanga hao ni pamoja na Maafisa Utawala wa Polisi watano na polisi watatu wakujitolea.

Vyombo vya usalama vimesema kuwa gari walilokuwa wanatumia marehemu hao lilikanyaga bomu la kutengenezwa kienyeji na gari hilo kurushwa angani.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema gari hilo liliharibiwa vibaya sana na watu wote waliokuwa ndani yake waliuwawa.

Mratibu wa eneo la Kaskazini Mashariki Muhammad Saleh amesema wale waliohusika na shambulizi hilo walikimbia mara baada ya tukio hilo.

Amesema uchunguzi wa awali unaashiria kuwa waliohusika ni kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab cha Somalia.

Shambulizi hili limekuja kufuatia tahadhari iliyotolewa kuwa kulikuwa na mpango wa shambulizi hili lililotolewa na kikundi cha kigaidi. Vyombo vya usalama wiki iliyopita vilitahadharisha kuwa magaidi wanapanga kufanya shambulizi kabla ya kumalizika mwezi wa Ramadhan.

XS
SM
MD
LG