Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 10:46

Al-Shabaab yadai kuhusika na mlipuko Mogadishu uliouwa 6


Hali ilivyokuwa kwa raia na magari ambayo yaliharibiwa kabisa na mlipuko wa bomu uliotokea Wilaya ya Hodan, Mogadishu,
Hali ilivyokuwa kwa raia na magari ambayo yaliharibiwa kabisa na mlipuko wa bomu uliotokea Wilaya ya Hodan, Mogadishu,

Maafisa wa serikali mjini Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, wanasema bomu liliripuka katika jengo la makao makuu ya wilaya na kuuwa watu wasio pungua sita na kujeruhi wengine 16.

Mlipuko huo ulikuwa umelenga makao makuu ya wilaya ya Hodan huko Mogadishu. Video iliyochukuliwa kwa kutumia simu kwenye eneo hilo inaonyesha wingu kubwa linalotokana na mlipuko ambao ulifika juu sana hewani.

Walioshuhudia wamesema mlipuko huo Jumatatu na kusababisha uharibifu mkubwa katika jengo la makao hayo makuu.

Afisa wa polisi Ibrahim Mohamed ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP, “Mlipuko huo ni mkubwa.”

Kikundi cha wapiganaji wa al-Shabaab kimedai kuhusika na shambulizi hilo kwa kutuma ujumbe kupitia wenye akaunti yao ya mitandao ya jamii.

Hii ni mara ya pili kikundi hicho kimelenga ofisi za makao makuu ya wilaya, Mogadishu mwezi wa Septemba.

Mnamo Septemba 2, gari la kujitoa muhanga liliharibu ofisi ya makao makuu ya wilaya ya jirani wa Hawlwadag, na kuuwa watu watatu.

XS
SM
MD
LG