Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:49

Polisi Kenya wazuia shambulizi kubwa la kigaidi


Waziri Fred Matiang'i
Waziri Fred Matiang'i

Polisi nchini Kenya wamezuia shambulizi la kigaidi lisitokee baada ya kupambana na watu wenye silaha na kumuua mmoja na kuwakamata wengine wawili.

Vyanzo vya habari nchini Kenya vimeripoti kuwa operesheni hiyo ilifanyika baada ya kugundua mrundiko wa silaha yakiwemo mabomu ya mkononi 36 na silaha aina ya rifle tano.

Maafisa hao walikamata gari la magaidi hao ambalo lilikuwa limeandaliwa tayari na vilipuzi.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa gari hilo lilikuwa linaelekea Nairobi ambako magaidi hao walikuwa wamepanga kutumia gari hilo lililokuwa limesheheneshwa na vilipuzi hivyo, kwa kifupi ilikuwa ni bomu lenye magurudumu.

Uchunguzi zaidi unaonyesha kuwa gari hilo lilikuwa limetengenezwa na vilipuzi hivyo na wataalamu wa kutengeneza mabomu wa al-Shabaab huko eneo la El-Adde, nchini Somalia.

Kufuatia mapambano hayo ya kutupiana risasi kati ya polisi na magaidi Alhamisi usiku katika eneo la Merti, Kaunti ya Isiolo, operesheni kubwa ya polisi inaendelea kuwasaka magaidi hao ktika jiji kwa nia ya kuwakamata wale wote walioshirikiana na magaidi hao.

Ripoti ya awali iliyotumwa kwa vyombo vya usalama ambayo gazeti la nation Kenya imeiona inasema kuwa magaidi hao huenda walikuwa wamekodi chumba katika hoteli moja kwa sababu walikuwa wanaufunguo, ambao ulikuwa na namba ya chumba cha hoteli hiyo.

Kwa sababu za operesheni za usalama zinazoendelea gazeti hilo limesema haliwezi kutaja jina la hoteli hiyo.

XS
SM
MD
LG