Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:27

Shambulizi la Kigaidi Somalia : Watu kumi wauawa


Mlipuko mkubwa wabomoa majengo nchini Somalia Februari 4, 2019.
Mlipuko mkubwa wabomoa majengo nchini Somalia Februari 4, 2019.

Kikundi cha Kiislam cha al-Shabaab kimedai kuhusika na mashambulizi mawili siku ya Jumatatu nchini Somalia ambapo raia tisa na mmoja wa kigeni walipoteza maisha.

Vyombo vya usalama nchini Somalia Jumatatu vimesema mlipuko mkubwa katika mji mkuu wa Somalia uliuwa watu hao tisa.

Afisa polisi Ahmed Moalin Ali ameiambia AFP kuwa magaidi walikuwa wamepaki gari iliyokuwa imesheheni vilipuzi karibu na eneo la biashara “ili kuwauwa raia wasiokuwa na hatia.”

AFP imesema al-Shabab imesema inahusika na shambulizi hilo katika mji mkuu ambalo liliwekwa kwenye mtandao wa kikundi chenye kuwasaidia al-Shabaab.

Wakati huohuo kikundi hicho cha kigaidi kimesema mmoja wa washambuliaji wake alitumia bunduki kumuuwa meneja wa bandari inayomilikiwa na Dubai katika mkoa unaojitawala wa Puntland. Watu wengine watatu walijeruhiwa katika tukio hilo.

Mohamad Dahir, afisa usalama wa eneo, ameliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP), “mtu mmoja alimpiga risasi na kumuuwa Paul Anthony Formosa ambaye alikuwa meneja wa ujenzi kwa kampuni ya DP World. Meneja huyo aliuawa ndani ya bandari hiyo na vyombo vya usalama pia walifanikiwa kumuuwa muuwaji huyo hapohapo.

“Sisi ndio tuliopanga operesheni hiyo,” Abdiasis Abu Musab, msemaji wa al-Shabaab ameliambia shirika la habari la Reuters. “Sisi tulikuwa tumemuonya meneja huyo, lakini alitupuuza. Alikuwa nchini Somalia kinyume cha sheria.”

Tamko la al-Shabaab lilieleza kuwa shambulizi hilo ndani ya bandari ilikuwa ni “sehemu ya operesheni pana inayolenga kampuni za mamluki ambazo zinaiba rasilmali za Somalia.

DP imesaini mkataba wa miaka 30 kuendeleza bandari hiyo ya Bosaso. Ripoti za Shirika la habari la AP zinasema mkataba huo wa maendeleo unathamani ya dola milioni 336.

XS
SM
MD
LG