Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:39

Watatu wakutikana na hatia katika shambulizi la kigaidi Garissa 2015


Wafanyakazi wakiweka majina ya wahanga wa shambulizi la Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2, 2016 ikiwa ni kumbukumbu kwa chuo hicho.
Wafanyakazi wakiweka majina ya wahanga wa shambulizi la Chuo Kikuu cha Garissa Aprili 2, 2016 ikiwa ni kumbukumbu kwa chuo hicho.

Mahakama moja nchini Kenya Jumatano imewakuta watu watatu wanamakosa ya kuwasaidia wapiganaji wa Somalia waliofanya mashambulizi Chuo Kikuu cha Garissa 2015 upande wa kaskazini mashariki mwa Kenya ambapo watu 148 waliuawa.

Mtu wanne aliachiwa huru, amesema Jaji Francis Andayi, akiongeza kuwa hukumu ya watu hao itatolewa Julai 3, 2019.

Watu hao watatu ni Mohamed Ali Abikar, Hassan Edin Hasaan wananchi wa Kenya na Rashid Charles Mberesero, Mtanzania – “walikuwa wanachama wa kikundi cha kigaidi cha al-Shabaab ambacho wanachama wake walifanya mashambulizi hayo,” ameeleza Andayi.

Shambulizi la Aprili 2, 2015 lilifanywa na watu wanne wenye silaha kutoka kikundi cha al-Shabaab, chenye mafungamano na al-Qaeda yenye makao yake Somalia.

Wengi ya wale waliouawa walikuwa wanafunzi, waliopigwa risasi wakiwa katika mabweni yao au kuzungukwa na kuuawa katika eneo la malazi yao.

Washambuliaji hao kwanza waliwapambanua wahanga hao kwa mujibu wa dini zao, wakiwaacha Waislam kuondoka na wengine walilazimishwa kubaki, wengi wao wakiwa Wakristo.

Hilo lilikuwa shambulizi la pili kubwa la umwagaji damu la kigaidi katika historia ya Kenya, na kubwa zaidi ya hilo ni shambulizi la ubalozi wa Marekani Nairobi 1998 ambalo liliua watu 213. Katika Shambulizi hilo al- Qaeda ilidai kuhusika.

Waendesha mashtaka walikuwa wamethibitisha “bila ya wasiwasi wowote” kuwa “washtaikwa hao walikuwa wanajua mpango huo,” amesema, lakini hakutoa maelezo yeyote juu ya madai ya hujuma hiyo.

Kukutikana kwa hatia kwa watu hao watatu ni tokeo la kwanza linalotokana na uchunguzi na mashtaka yaliyochukuwa muda mrefu.

Katika shambulizi hilo watu wote wanne waliokuwa na silaha waliuawa na vikosi vya usalama. Kiongozi kinara mshukiwa wa operesheni hiyo, Mohamed Mohamud, pia kwa jina la “Kuno,” mwalimu wa zamani wa madrasa ya Quran huko Garissa, aliuawa upande wa kusini magharibi ya Somalia 2016.

Kikundi cha al –Shabaab kimesema aliuawa na wapiganaji wanaotaka “mfumo kristo” kutoka Marekani.

Kikundi hicho cha al-Shabaab kinapigana kuipindua serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa Mogadishu.

Kikundi hicho pia kimekuwa kikifanya mashambulizi katika nchi jirani ya Kenya, ambayo ina vikosi vya jeshi lake Somalia ikiwa ni sehemu ya jeshi la Umoja wa Afrika.

XS
SM
MD
LG