Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:48

Al-Shabaab waharibu nguzo ya mawasiliano, wateka waalimu Garissa


Wapiganaji wa al-shabaab
Wapiganaji wa al-shabaab

Wapiganaji wa al-Shabaab wameshambulia na kuharibu nguzo ya shirika la Simu la Safaricom katika eneo la Fafi, kaunti ya Garisaa na kufanya eneo hilo lisiweze kuingilika kwa muda.

Tukio hilo limetokea Jumatano usiku na washambuliaji hao wanasadikiwa kuwa waliweka mabomu katika njia inayoelekea katika eneo hilo.

Polisi walichelewa kufika kwenye eneo hilo kwa hofu ya kuathiriwa na mabomu yaliyokuwa hayajulikani yamepandikizwa sehemu gani katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Mashariki Mohamed Saleh amesema wamepeleka timu ya maafisa wa polisi kwenye eneo hilo ili kufanya tathmini juu ya uharibifu huo.

“Tunajua kuna maharamia ambao wameharibu nguzo ya mawasiliano katika kituo cha Fafi na kuyumbisha shughuli mbalimbali hapo. Lakini tunawafuatilia,” amesema kamanda huyo.

Polisi hawakuweza kuthibitisha repoti kwamba wapiganaji hao walichoma moto shule ya msingi katika eneo hilo.

Wakazi waeneo hilo wamesema kuwa wapiganaji hao waliwateka waalimu wawili katika shule hiyo ilioshambuliwa.

Waalimu hao wanasemekana kuwa sio wakazi wa eneo hilo. Hata hivyo haijulikani wapi walipo. Wapiganaji katika wiki za karibuni wameendeleza mashambulizi yao katika eneo hilo na kuua sio chini ya maafisa usalama 20.

Mashambulizi hayo yaliolenga nguzo ya mawasiliano ni la hivi karibuni katika mtiririko wa mashambulizi yaliotokea katika eneo likiacha athari ya uharibifu mbalimbali.

Maeneo mengine ambapo nguzo hizi zimeharibiwa ni pamoja na Mandera na Wajir.


XS
SM
MD
LG