Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:46

Maeneo yaliosahaulika Kenya yenye mauaji ya kutisha


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa, wakazi wa maeneo ya Mandongoi, Mwanzele na Kasiluni yaliyoko katika kaunti ya Kitui karibu na mpaka wa kaunti ya Tana River wamekatishwa tamaa.

Wamekatishwa tamaa kutokana na kutokuwepo amani, wakati wakiendelea kukabiliana na hali ya mashambulizi yanayoendelea yakitokana na wafugaji.

Mara kwa mara, wafugaji wenye silaha kutoka kaunti zaTana River, Garissa, Wajir na Mandera wanavuka kuja eneo la Kitui wakiwa na maelfu ya mifugo yao wakitafuta malisho, wanawashambulia wakulima maskini na kuacha athari za vifo, majeruhi na uharibifu.

Kwa mujibu wa gazeti la Standard la Kenya mwaka uliopita peke yake, watu 33 waliuawa na kati yao wengine kwa namna za ukatili uliokiuka mipaka.

Mbali na kupigwa risasi, wengine hasa wanaume, wanakatwa vichwa kwa mapanga na vichwa vyao kuchukuliwa.

Shambulio la hivi karibuni lilitokea wiki moja iliyopita wakati watu watatu walipovamia na kuuwa kinyama.

Watu wawili kati yao walipigwa risasi na kuuawa wakati wanalisha mifugo na mtu wa tatu alishambuliwa kwenye shamba lake na kukatwa kichwa.

Chifu wa Kavani Timothy Kimwele amesema wakazi hao sasa wanaishi kwa hofu kwa sababu wafugaji wenye silaha nzito nzito wanashambulia bila kutarajiwa.

Takriban familia 1,000 zimelazimishwa kuacha makazi yao na wanakaa katika makambi huko msituni wakikabiliwa na hali mbaya sana.

Kufuatia mashambulizi hayo ya mara kwa mara yanayofanywa na maharamia hao, na ambayo yanachochewa na kupigania maji na maeneo ya malisho ya Wanyama, baadhi ya shule katika eneo hilo zimefungwa wakati watoto, wazazi na walimu wamelazimika kukimbia ili kuzisalimisha nafsi zao.

Katika shule ya msingi ya Mandongoi huko Mwingi upande wa Kaunti ndogo Kaskazini, ambayo iko katika “ukanda wa mauaji” ambao umezingirwa na maharamia hao na kufanya wanavyotaka, na hivyo basi wazazi wamewazuia wanafunzi 450 wa shule ya msingi kutohudhuria masomo kwa hofu ya mauaji.

XS
SM
MD
LG