Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 09:49

Shambulizi la Kigaidi Kenya :Washukiwa sita wafikishwa mahakamani


Washukiwa kutoka kushoto, Osman Ibrahim, Oliver Muthee, Gladys Kaari, Guled Abdihakim na Joel Nganga wakiwa kizimbani katika Mahakama ya Mililani wakikabiliwa na shutuma za kufanya shambulizi katika eneo la biashara la DusitD2 complex, in Nairobi, Kenya, Jan. 18, 2019.
Washukiwa kutoka kushoto, Osman Ibrahim, Oliver Muthee, Gladys Kaari, Guled Abdihakim na Joel Nganga wakiwa kizimbani katika Mahakama ya Mililani wakikabiliwa na shutuma za kufanya shambulizi katika eneo la biashara la DusitD2 complex, in Nairobi, Kenya, Jan. 18, 2019.

Washukiwa sita, akiwemo raia wa Canada, wamefikishwa mahakamani Ijumaa nchini Kenya, kuhusiana na shambulizi la kigaidi kwenye hoteli moja mjini Nairobi na kusababisha vifo vya watu 21.

Watuhumiwa hao wametajwa kuwa Joel Ng’ang’a Wainaina, Oliver Kanyango Muthee, Gladys Kaari Justus, Osman Ibrahim, Hussein Muhamed na Guleid Abdihakim ambaye ni raia wa Canada.

Jaji wa mahakama alikubali ombi kutoka kwa upande wa mashtaka kutaka watuhumiwa hao wanne na mwanamke mmoja kubaki chini ya ulinzi kwa siku 30 wakati uchunguzi ukiendelea. Mtuhumiwa wa sita atafikishwa mahakamani wiki ijayo.

Watuhumiwa wanashutumiwa kuhusu ‘uwezekano wa kuhusika’ katika shambulizi la takriban saa 20 kwenye hoteli ya Dusit D2 na jengo la ofisi ambalo mshambuliaji bomu wa kujitoa mhanga na watu wanne walio kuwa na silaha waliuawa na majeshi ya usalama, nyaraka iliyotolewa mahakamani imesema.

“Uchunguzi kuhusiana na suala hili una mambo mengi na ni wa kimataifa na huenda ukahitaji muda zaidi na rasilimali ili kubaini mtandao mzima wa kihalifu,” taarifa kutoka kwa mkurugenzi wa mashtaka, Noordin Haji imesema.

Washukiwa 11 walikamatwa Jumanne baada ya shambulizi, hata hivyo uchunguzi kuhusiana na washukiwa wengine bado unaendelea.

Mtuhumiwa Wainaina anadaiwa ni dereva wa taxi ambaye aliwapatia usafiri washambuliaji mara kadhaa sehemu mbali mbali mjini, na Muthee ni dereva mwingine ambaye aliwapeleka baadhi ya washambuliaji kwenye eneo la tukio.

Mwanamke pekee katika kundi hili la watuhumiwa Gladys Justus anachunguzwa kwa kuhusika katika kutuma fedha, wakati raia wa Canada, Guleid Abdihakim anachunguzwa kwasababu ya mawasiliano yake na baadhi ya watuhumiwa.

Ibrahim anadaiwa kuwa alikutana na mmoja ya washambuliaji Januari 8.

Muhamed simu yake ilionyesha mawasiliano na baadhi ya wanamgambo wa kiislamu na atafikishwa mahakamani wiki ijayo siku ya Jumatano.

Washukiwa wawili bado hawajafikishwa mahakamani, Ali Salim Gichunge na Violete Kemunto Omwoyo ambayo wana kadi za simu ambazo zinaonyesha walikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara na baadhi ya namba nchini Somalia, nyaraka za mahakama zimeonyesha.

Shambulizi ambalo inadaiwa lilifanywa na kundi la wanamgambo wa kiislamu la al-Shabaab la Somalia, lenye uhusiano na al-Qaeda limehusika kuilenga Kenya mara kwa mara katika mashambulizi.

Mwaka 2013 kundi hilo lilifanya shambuliz kwenye eneo la maduka la Westgate mjini Nairobi na kusababisha watu 67 kupoteza maisha, wakati mwaka 2015 kundi hilo liliua watu 18 katika chuo kikuu cha Garissa, mashariki mwa Kenya.

XS
SM
MD
LG