Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 21:03

10 wauliwa Somalia baada ya kiongozi wa Al-Shabaab kuuwawa


Mashahidi kwenye mji mkuu wa Somalia wamesema takriban watu 10 wameuwawa na wengine zaidi ya 15 kijeruhiwa baada ya wanamgambo kushambulia hoteli moja maarufu Jumatano.

Majeraha mengi yanasemekana kusababishwa na bomu la kwenye gari lililoteguliwa nje ya hoteli ya Ambassador mjini Mogadishu wakati watu wengi walipokuwa wakihudhuria sala za jioni.

Mjumbe wa Somalia, Mohamed Ismail Shuriye, ameambia VOA kuwa wajumbe wawili, Abdullahi Jama Kaboweyne na Mohamud Gure, wameuwawa kwenye shambulizi hilo.

Ameongeza kusema kuwa mjumbe wa Abdullahi Hashi amejeruhiwa.

Shambulizi hilo limetokea saa chache baada ya mmoja wa makamanda wa Al- Shabaab kuuwawa usiku wa kuamkia jumatano.

Mohamed Mohamud anaejulikana pia kama Dulyaden, anashukiwa kupanga mashambulizi ya Aprili 2015 kwenye chuo kikuu cha Garissa nchini Kenya ambapo watu 148 wengi wao wakiwa wanafunzi waliuwawa.

XS
SM
MD
LG