Kwa karibu mwaka mzima Tanzania imedai hakuna corona nchini humo, na kuwa nchi pekee Afrika Mashariki ambayo haina masharti rasmi ya kujikinga na ugonjwa huo.
Matukio ya siku za hivi karibuni - kuanzia idadi ya vifo isiyo ya kawaida, matamshi ya baadhi ya viongozi wa kijamii, kidini, wapinzani wa kisiasa na simulizi za wananchi yameonyesha dalili kwamba ugonjwa huo upo nchini Tanzania na huenda unaenea kwa kasi kubwa.
Serikali ya Tanzania hadi sasa inashikilia msimamo ambao mara kwa mara unarudiwa na Rais John Pombe Magufuli kuwa corona haipo Tanzania kufuatia maombi ya kitaifa yaliyofanywa mwaka 2020.
Rais Magufuli Jumatano aliongeza sintofahamu miongoni mwa wananchi kwa kuwataka Watanzania wachukue tahadhari bila kusema endapo ugonjwa huo upo nchini ama la.
Lakini baada ya miezi kadha taasisi za kiafya, kidini, na wananchi wa kawaida kukubali matamshi ya serikali kwamba Corona haipo Tanzania, siku za hivi karibuni zimeonyesha picha tofauti.
James Mbatia ni kiongozi wa upinzani ambaye amekuwa miongoni mwa wanasiasa wa kwanza kutamka hadharani kwamba kuna ishara nyingi za kuwepo corona Tanzania
Your browser doesn’t support HTML5
Kwa namna fulani Rais Magufuli alikiri Jumatano kwamba kuna aina mpya ya virusi vya corona Tanzania, akidai kuwa vilimeletwa na watanzania waliopata chanjo nje ya nchi. LakTaini alisema pia Tanzania haitakubali chanjo ya Covid-19 bila kwanza kufanyiwa tathmini na wizara ya afya ya nchi hiyo.
Your browser doesn’t support HTML5
Wiki hii kanisa katoliki – moja ya taasisi kubwa za dini nchini Tanzania – lilitoa tahadhari juu ya wimbi jipya la maambuziki ya corona katika nchi jirani na kuwataka wananchi kuchukua kila aina ya tahadhari kujikinga na maambukizi hayo. Waraka wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Katoliki Tanzania (TEC) Askofu Gervas Nyaisonga hakusema moja kwa moja kama maambuziki hayo yapo nchini tanzania.
Vile vile, Wizara ya Afya nchini humo, bila kukiri uwepo wa ugonjwa huo, ilitoa maelekezo ya tahadhari za kuchukua kwa watu wanapokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kunawa mikono, kuepuka msongamano – yote masharti ambayo tangu awali yanatolewa kujikinga na corona.
Zitto Kabwe ni miongoni mwa viongozi wa upinzani waliozungumzia wasiwasi wa kuwepo au kuongezeka kwa maambukizi ya corona Tanzania.
Your browser doesn’t support HTML5
Ripoti za kwenye mitandao ambazo haraka zilikanushwa na waliozitoa au maafisa wa serikali zimedai kuwa hospitali kadha zina ongezeko la wagonjwa wenye matatizo ya kupumua. Maafisa wa afya nchini Tanzania wamekuwa wakizungumzia tatizo la watu kukabiliwa na hata kufariki kutokana na ugonjwa wa kushindwa kupumua vizuri – nimonia – bila kuhusisha tatizo la kupumua na corona.
Katika jamii nchini Tanzania kumekuwa na ongezeko lisilo la kawaida la vifo ingawa vifo hivyo havihusishwi rasmi na corona. Tanzania iliacha kutoa takwimu za wagonjwa wa corona Mei mwaka jana, na kutangaza kuwa ni viongozi wa juu pekee – rais, waziri mkuu, waziri wa afya na msemaji wa serikali (sic)– ndio wazungumzaji pekee kuhusu hali ya corona nchini humo. Kwa mara nyingine tena, kiongozi wa upinzani Zitto Kabwe.
Your browser doesn’t support HTML5
Wananchi pia inaelekea wanachukua hatua zao binafsi za tahadhari. Miezi michache iliyopita haikuwa kawaida kuona watu wakiwa wamevaa barakoa nchini Tanzania lakini katika siku chache zilizopita baadhi ya watu wamerejea kuvaa barakoa, kuosha mikono na kuepuka misongomano.
Your browser doesn’t support HTML5
Maafisa wa afya, madaktari na hospitali hazitoi matamshi yoyote kuhusu ugonjwa wa corona licha ya ripoti zinazovuja kwamba baadhi ya hospitali zina wimbi la ugonjwa huo katika wodi zake.