Lema na familia yake wamekuwa wakiishi nchini Kenya kwa takriban mwezi mmoja.
Mapema mwezi jana, Lema, mbunge wa zamani wa jimbo la Arusha mjini, alidaiwa kukamatwa, wakati akikimbilia nchini Kenya pamoja na familia yake, kwa kile alichoeleza ni kwa ajili ya usalama wake.
Vyombo vya habari vya Kenya viliripoti kuwa Lema alikamatwa Ilbissil Kaunti ya Kajiado baada ya yeye na familia yake kuvuka kupitia mpaka wa Namanga.
Mbunge huyo alikamatwa na polisi jijini Dar es Salaam Novemba Mosi, 2020 akiwa pamoja na wanasiasa wengine wa upinzani.
Baadaye mashirika ya kutetea haki za binadamu yalianza kuishinikiza Kenya kumpa hifadhi ya kisiasa. Mwanasiasa huyo amekuwa mmoja wa viongozi wa upizani, ambao walilalamikia vikali matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba nchini Tanzania, wakidai kwamba ulijawa na dosari za kila aina.
Lema ambaye anahamia Canada Pamoja na familia yake, alihudumu kama mbunge wa Arusha Mjini kutoka mwaka wa 2010 hadi 2020.