Katika kituo kimoja cha afya wiki iliyopita, mama na mtoto wake mchanga aliyekuwa na uzito wa paundi 1.7 tu walifariki dunia kutokana na njaa.
Katika kila wilaya zaidi ya 20 ambako kikundi kimoja cha misaada kinafanya kazi, wakazi wamekufa kwa njaa.
Kwa miezi kadhaa, Umoja wa Mataifa, UN, umeonya juu ya njaa katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia ambalo limekumbwa na matatizo, na kuuita ni mzozo mbaya sana wa njaa duniani kwa kipindi cha miaka kumi.
Nyaraka za ndani na maelezo ya mashuhuda yanabaini vifo vya kwanza kutokana na njaa tangu serikali ya Ethiopia mwezi Juni ilipoweka kile Umoja wa Mataifa inakiita kizuizi cha misaada ya kibinadamu.
Njaa ya kulazimishwa ndio sura mpya ya hivi karibuni katika mzozo ambapo watu wa kabila la Tigray wameuawa, kubakwa na magenge ya watu na kufukuzwa.
Miezi baada ya mazao kuchomwa moto na jamii kunyanga’anywa kila kitu aina mpya ya vifo imeanza kutokea.