Baada ya watu 7 kuuawa Alhamisi katika eneo la Mbau, mjini Beni, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wananchi wamepaza sauti wakiitaka serikali yao kuomba msaada.
Wabunge katika miji ya Beni na Butembo wanataka serikali ya Rais Felix Tshisekedi, kuomba msaada wa kimataifa kukabiliana na uhalifu.
Hili linatokana na kuwepo kwa makundi ya uhalifu yanayoendelea kutekeleza mauaji hayo, Kivu kaskazini.
Wabunge hao, pia wametoa wito kwa nchi zenye nguvu duniani kuwa mstari wa mbele katika kupambana na makundi ya waasi.
Wamedai kuwa jeshi la Umoja wa Mataifa MONUSCO, limeshindwa kurejesha amani katika eneo hilo.
Imetayarishwa na mwandishi wetu Austere Malivika, DRC.