Kwa mujibu wa Jenerali Bruno Mandevu mapambano kati ya wanajeshi wa Rwanda na wanajeshi wa DRC yaliyojiri katika mbuga za Wanyama, Virunga nchini DRC, yalisababisha mauaji hayo.
Hata hivyo Serikali ya Rwanda imekana madai kwamba jeshi lake lilihusika na mauaji hayo.
Mandevu ameongeza kuwa wanajeshi wa Kongo walifikiria kuwa wanapambana na waasi walioko katika eneo hilo.
Kwa mujibu ya wachambuzi wa mambo ya kisiasa wengi wanahofia mapigano hayo yanaweza kupelekea hali zaidi ya kutoaminiana ambayo inajiri kwa muda mrefu sasa.
Shirika la habari la BBC limeripoti kuwa msemaji wa jeshi la Rwanda kanali Innocent Munyengango amethibitisha kutokea kwa mapambano hayo na kusema hakukuwa na majeruhi wowote kwa upande wa Rwanda.
''Jeshi la Congoleese lilivamia kambi yetu na kutushambulia. Wanajeshi wetu walilazimika kujitetea'', alisema.