Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:40

Waasi 11 wa DRC wafungwa maisha kwa ubakaji


Wanamgambo katika jimbo la Kivu Kusini, nchini DRC (VOA/Charly Kasereka)
Wanamgambo katika jimbo la Kivu Kusini, nchini DRC (VOA/Charly Kasereka)

Wanachama kumi na mmoja wa kundi la wanamgambo nchini DRC Jumatano walihukumiwa kifungo cha maisha gerezani baada ya kupatikana na hatia ya kuwabaka  watoto dazeni ya watoto, na mauaji.

Asasi za kutetea haki za binadamu zilisifu hukumu hiyo na kuitaja kuwa ya kihistoria katika nchi ambayo ina visa vingi vya manyayaso ya ngono ambayo mara nyingi wanaoyatekeleza hawaadhibiwi.

Taarifa iliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Physicians for Human Rights, ilisema kuwa kwa muda mrefu sana, wabakaji nchini Kongo wamekuwa wakijiona kama wasioweza kuwajibishwa kisheria na kuongeza kwamba polepole, taswira hiyo imeanza kubadilika.

Washukiwa waliaminika kuwa wanamgambo wa kundi linalojiita "Jeshi ya Yesu," wakiongozwa na mbunge wa jimbo la Kivu Kusini, Fredric Batumike.

Mahakama hiyo aidha iliamuru kila muathiriwa alipwe fidia ya dola elfu tano, na dola 15,000 kwa familia ambazo jamaa zao waliuawa kwa kupinga au kushutumu vitendo vya waasi.

Shirika hilo lilisema hii ni mara ya kwanza kwa afisa anyehudumu serikalini kupatikana na hatia ya kuwajibika pakubwa kwa vitendo vya uhalifu uliotekelezwa na waasi, ambao aliwadhibiti na kuwafadhili.

XS
SM
MD
LG