Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 03:16

Balozi Nikki Haley amemtumia ujumbe mzito Rais Kabila wa DRC


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley. Jan. 2, 2018.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley. Jan. 2, 2018.

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Nikki Haley, Jumatatu alimuomba waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC kupeleka ujumbe kwa Rais Joseph Kabila wa DRC kuusu mauaji ya wachunguzi wawili wa Umoja wa Mataifa, ujumbe huo unasomeka “tafadhali muulize bwana Kabila kile alichokifanya na orodha yangu”.

Balozi Nikki Haley (L) na Rais Joseph Kabila wa DRC. Oktoba 2017
Balozi Nikki Haley (L) na Rais Joseph Kabila wa DRC. Oktoba 2017

Kulingana na ripoti ya shirika la habari la Reuters orodha ambayo Haley alimwambia Kabila wakati alipokutana naye mjini Kinshasa mwezi Oktoba mwaka 2017 ilitaja majina ya watu waliohusika katika mauaji ya Zaida Catalan na Michael Sharp mwezi Machi mwaka 2017 ilisema ofisi ya Marekani katika Umoja wa Mataifa.

Balozi Haley alimweleza Rais Kabila kwamba sheria kuhusiana na mauaji hayo ilikuwa kipaumbele cha Marekani, ofisi ya Marekani ilisema hivyo. Sharp ambaye ni raia wa Marekani na Catalan raia wa Sweden waliuwawa huko kati kati ya Congo wakati wakifanya uchunguzi huru kwa ripoti inayokwenda baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Miili ya Sharp na Catalan ilipatikana kwenye kaburi wiki mbili baadae.

XS
SM
MD
LG