Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:38

Amnesty International yasimamia msamaha wa waasi 27,438 Uganda


Amnesty İnternational
Amnesty İnternational

Takriban waasi 27,438 nchini Uganda, wamepewa msamaha na shirila la haki za binadamu la kimataifa Amnesty International, kwa niaba ya serikali.

Mwenyekiti wa Amnesty International nchini Uganda Jaji mstaafu Peter Onega, amesema idadi kubwa ya waliosamehewa (13,291) wanatoka kundi la Lord’s Resistance Army – LRA, linaloongozwa na Joseph Kony.

Wengine wanatoka makundi ya waasi ya West Nile Bank Front – WNBF (6,500), National Rescue Front – UNRF (3,252) na Allied Democratic Forces - ADF (2,315), ambalo muasisi wake ni Jamil Mukulu mwenye umri wa miaka 55, anayezuiliwa Uganda baada ya kukamatwa nchini Tanzania, April mwaka 2015.

ADF yataka mazungumzo na serikali

Onega amesema uongozi wa kundi la ADF unataka kufanya mazungumzo na serikali ili kumaliza uasi wa miaka 22, akifafanua kwamba kundi hilo lilimteua kiongozi mwingine baada ya kukamatwa kwa Jamil Mukulu, na kwamba Amnesty International imekuwa ikifanya mazungumzo na kundi hilo tangu mwaka 2008.

Office ya Amnesty International ya Uganda, bado inashughulikia maombi ya waasi 5,671wanaotaka msamaha wa serikali.

Onega amesema kwamba serikali ya rais Yoweri Museveni ipo tayari kwa mazungumzo na kundi hilo la ADF ambalo linaaminika kujificha nchini jamhuri ya kidempkrasia ya Congo na kushutumiwa kutekeleza mauaji ya watu mashuhuri nchini Uganda akiwemo mbunge Ibrahim Abiriga, na mwendesha mashtaka Joan Kagezi.

Kikundi cha ADF

Ni kundi lililoundwa na Jamil Mukulu mwaka 1989, mashariki mwa Uganda. ADF liliundwa kupinga kile kinachotajwa kama kutengwa na serikali katika maendeleo

Dhamira ya kundi hilo ni kupindua utawala wa Rais Yoweri Museveni pamoja na kuanzisha utawala wa Sharia ya Kiislam nchini Uganda.

Kundi hilo limekuwa Likifanya uasi dhidi ya serikali ya Uganda upande wa mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ( DRC).

Limeshutumiwa kutekeleza mauaji mengi Uganda hususan dhidi ya maafisa wa ngazi ya juu serikalini. Linaaminika kuwa na wapiganaji wasiozidi 500.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Kennes Bwire, Washington, DC

XS
SM
MD
LG