Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:38

Miili ya wanajeshi 14 wa Tanzania kuwasili leo


Mkuu wa Jeshi la Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibola
Mkuu wa Jeshi la Tanzania Luteni Jenerali James Mwakibola

JESHI la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limesema kuwa miili ya askari 14 wa Jeshi hilo waliouawawa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inatarajiwa kuwasili nchini Jumatatu jioni.

Mnadhimu Mkuu wa JWTZ, Luteni Jenerali James Mwakibola anaelezea shambulizi la Disemba 7, halijaivunja moyo Tanzania katika operesheni zake za amani.

Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi huyo shambulizi hilo dhidi ya askari wake wanaolinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni baya na halijawahi kutokea tangu vikosi vyake vianze kushiriki Ulinzi wa Amani huko kupitia Umoja wa Mataifa mwaka 2011.

Kutokana na shambulio hilo lililodumu kwa saa 13, JWTZ imepoteza askari 14 na wengine 44 wamejeruhiwa, wawili wakiwa hawajulikani walipo na jitihada za kuwatafuta zinaendelea.

Luteni Jenerali Mwakibolwa amesema shambulio lililotokea DRC ni shambulio ambalo kwa mara ya kwanza jeshi hilo liliamua kutoa taarifa. Ameeleza kuwashambulio hilo limeleta madhara makubwa.

Hata hivyo amesema kuwa kikosi chao kilichopo DRC bado kina uwezo wa kutekeleza majukumu kwa uhodari, ushupavu, weledi na umahiri stahiki.

Wakati huohuo vyanzo vya habari vimeeleza kuwaJWTZ na Serikali ya Tanzania zinaendelea kuchukua hatua stahiki ikiwemo kufanya uchunguzi katika eneo husika.

Desemba 07, mwaka huu jioni sehemu ya Kikosi cha askari wa JWTZ kilichopo DRC kulinda amani kilivamiwa na waasi wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) katika kambi ndogo iliyopo eneo la daraja mto Simulike barabara ya kutokea Oicha kwenda Kamango mpakani mwa Uganda Kaskazini Mashariki ya Wilaya ya Beni, jimbo la Kivu Kaskazini. Hata hivyo, shambulio hilo la kuvizia lilizusha mapigano baina ya kikosi cha JWTZ na waasi hao ambapo askari wa JWTZ waliuawa na wengine kujeruhiwa vibaya. UN imethibitisha.

XS
SM
MD
LG