Uchaguzi wa Rais: Uchumi wa Marekani ni moja ya masuala makubwa sana kwa wapiga kura

  • VOA News

Matangazo ya kupiga kura “I Voted” zikiwa zimewekwa katika kituo cha kuhesabu na kupiga kura katika kaunti ya Maricopa (MCTEC) kabla ya uchaguzi wa awali huko Arizona 2024 na uchaguzi mkuu huko Phoenix, Arizona Juni 3, 2024.

Uchumi wa Marekani ni moja ya masuala makubwa sana kwa wapiga kura katika kinyang’anyiro cha urais mwaka huu kati ya Joe Biden and Donald Trump.

Rais wa Marekani Joe Biden

Biden alifanya kampeni wiki hii kuhusu uwekezaji katika teknolojia mpya. Trump anasema atazungumzia kuacha na matumizi ya Biden kwa miundo mbinu na kuongeza uchimbaji mafuta.

Kampeni ya Joe Bide kuhusu uwekezaji katika teknolojia wiki hii katika jimbo la Maghribi Kati la Wisconsin, ambako Microsoft inatumia dola bilioni 3.3 kwa kituo kipya cha data ambacho Biden anasema “ni mfano mwingine wa matumaini ya sekta binafsi.”

Rais Joe Biden anasema: “Hadi hivi sasa, tumetengeneza dola bilioni 866 katika uwekezaji wa sekta binafsi kote nchini, karibu matrilioni ya dola – kiwango cha kihistoria katika muda mfupi na kwa kinafunga milango ya maelfu ya ajira, kujenga viwanda vipya ya seminconductor, magari ya umeme na betri na mengine mengi zaidi, yote hapa Marekani.”

Eneo la kituo kipya cha data cha Microsoft ni same hiyo ambako miaka sita iliyopita Donald Trump alitangaza uwekezaji wa dola bilioni 10 uliofanywa na kampuni ya elektroniki ya Foxconn.

Eneo hilo lilitarajiwa kufungua nafasi mpya za ajira 13,000 kwa Wisconsin. Halikujenwa. Biden aliita ni ahadi nyingine iliyokuwa haikutimizwa kutoka kwa Trump.

Rais Joe Biden anaeleza: “Kwa hakika, amekuja hapa na Seneta wenu Ron Johnson, kwa kweli akiwa ameshika koleo la dhahabu, akiahidi kujenga maajabu nane ya dunia. Mnanitania? Angalia kilichotokea. Walichimba shimo na makoleo ya dhahabu, na halafu waliingia ndani.”

Trump anasema Biden hakuushughulikia vyema uchumi wa Marekani, akizungumzia kupanda kwa mfumuko wa bei kwa mwaka.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump akitoka mahakamani New York, Mei 30, 2024.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican alisema: “Uchumi haufanyi vizuri. Ndiyo tunaona mfumuko wa bei, uko juu mno. Hawatakuwa na uwezo wa kushusha viwango vya riba kama wanataka. Ni suala la kisiasa, lakini itakuwa mbaya sana kama wakifanya.”

Trump anafanya kampeni dhidi ya matumizi ya miundo mbinu yanayofanywa na Biden, ikiwa ni pamoja na nishati safi na teknolojia.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Nitakapochukua madaraka, nitasitisha kwa haraka ruzuku ya matumizi yote mapya na misaada iliyotolewa chini ya Joe Biden kwa mipango mikubwa ya kisoshalisti inayojulikana kama Inflation Reduction Act. Tutaziokoa fedha zote hizo.”

Biden anasema matumizi katika miundo mbinu yatasaidia uchumi wa Marekani.

Rais Joe Biden alisema: “Kwa kuongezea, barabara na barabara kuu na nyingine zaidi zitakuwa ni mali ya Marekani, zimejengwa na wafanyakazi wa Marekani, zitafungua ajira zinazolipa vizuri kwa Marekani.”

Trump anasema mipango yake ya kazi itajumuisha kuweka viwango katika uchimbaji mafuta na kuwalinda wafanyakazi wa Marekani kutokana na ajira haramu.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican alisema: “Mpango ni upi kwa ajira? Ndiyo, mpango wangu kwa ajira ni kuchimba, chimba tu, mshushe bei ya nishati, funga mpaka, waondoe wahalifu wote ambao wanaruhusiwa kuingia nchini kwetu.

Ukusanyaji maoni uliofanywa na Harvard CAPS – Harris unaonyesha kuwa mfumuko wa bei ni suala muhimu sana kwa wapiga kura Marekani, huku mtu mmoja kati ya watatu akisema uchumi uko katika mwelekeo sahihi.